Matokeo Kidato cha Nne 2012 ni FEKI (yamepikwa) - GREEN ACRES

Acheni ujinga wa kutafuta vijisababu vidogovidogo na kuvikuza ili kufunika ukweli halisi. Jadilini sababu za msingi. Hii ya Green Acres ni issue ndogo ukizingatia kuwa scripts za wanafunzi bado ziko pale NECTA. Mtu ambaye hakubaliani na matokeo anaweza kufika NECTA kuyahakiki. Tuangalie 60% ya wanafunzi kufeli, tatizo liko wapi? Kwa maoni yangu nikuwa watuwengi wanaojaribu kuelezea sababu ni wanafiki. Hawa gusii hata maslahi bora ya walimu, ambao ni wadau muhimu ktk mafanikio ya watoto. Watanzania sijui nani katudumaza kiakili, walimu wakilalamikia maslahi mabovu ya kazi yao, mazingira magumu ya kazi, serikali inatoa majibu mepesimepesi, sisi tunanyamaza tukiamini kwamba hayo ni matatizo ya walimu tu. Sasa tupokee, tukubali matokeo haya. Ni ununda wa hali ya juu kutegemea maziwa mengi mazuri kutoka kwenye ng'ombe usiemlisha vizuri. Akili za viongozi wetu na sisi wenyewe ziko wapi? Tuko bize kujenga wadarasa na kuyajaza wanafunzi bila walimu halafu tunashangaa matokeo. CCM wako bize kujisifia wameongeza vyumba vya madarasa wananchi tunapiga makofi na kukenua meno. Tuanze kuwahoji mambo kama haya. Tuacheni upuuzi sisiwananchi wa kawaida kwani ni watoto wetu wanaoathirika. Waviongozi wako international schools.
 
Kati ya mawaziri watalii kwenye baraza la mawaziri la Mh Kikwete ni Mh Shukuru Kawambwa na mwenzake Profesa Jumanne Magembe na ndio kati ya mawaziri ambao Wizara zao hazijatulia zina matatizo kila kukicha vurugu hamna maelewano na bado wanabebwa na Mkuu wa kaya,hii serikali ya kubebana ndio maana anasema hajiuzulu
 
NECTA yabanwa, yadaiwa kutoa matokeo ya
uongo
*Mwanafunzi apewa alama za juu bila
kufanya mtihani
BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limezidi
kuandamwa na kashfa, kutokana na matokeo ya
kidato cha nne ya mwaka 2012 yaliyotangazwa
juzi kuwa mabaya.
Kashfa hiyo inazidi kuchukua sura mpya
kutokana na udanganyifu mkubwa, ambapo
imebainika kuwa baadhi ya wanafunzi waliopata
alama za juu katika matokeo hayo hawakufanya
mitihani.
Taarifa hizo ziliibuliwa jana na Mkurugenzi wa
Shule ya Sekondari ya Green Acres, Julian
Bujugo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam juu ya matokeo hayo.
Bujugo, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Magomeni, jijini Dar es Salaam, alionyesha
kukerwa na matokeo hayo, huku akihoji
mazingira ya baadhi ya wanafunzi wa shule yake
kupatiwa alama za juu.
Katika mazungumzo yake, Bujugo alisema
wanafunzi wa shule yake wamefanyiwa mchezo
mchafu na baadhi ya watendaji wa Baraza la
Mitihani nchini, jambo ambalo limewaathiri
kisaikolojia.
Bujugo alisema katika matokeo hayo, wanafunzi
wake watatu wamekumbwa na tatizo hilo ambapo
mmoja wa wanafunzi hao, Amphey Sanga,
aliyefukuzwa shuleni hapo kabla ya kufanya
mitihani, alionekana kufanya vizuri kwa kupata
daraja la tatu na pointi 24 (Div 3.24)
“Baada ya kupata matokeo haya, tumefanya
uchambuzi wa haraka ambapo mwanafunzi
Amphey Sanga amepewa namba ya mtihani
01197/0148.
“Matokeo yake amepata masomo ya Civics- D,
Historia-D, Geograph-C, Kiswahili-D, Kiingereza-C,
Physics-D, Chemistry-C, Biology-C na Hesabu-D,
ambapo amepata Division 3.24.
“Tunashangaa huyu mwanafunzi amepataje alama
hizi hali ya kuwa hakufanya mtihani wa Taifa na
alifukuzwa hapa shuleni?,” alihoji Bujugo.
Matokeo mengine yanayoleta utata na kushangaza
ni kuhusu mwanafunzi aliyefanya mtihani huo wa
taifa, Martin Rushwangwa, mwenye namba ya
Mtihani 01197/0173, ambaye matokeo yake
yanaonyesha amepata daraja sifuri.
Mkurugenzi huyo alisema mwanafunzi huyo
alisaini kufanya masomo saba ya mchepuo wa
sanaa, lakini katika matokeo yake anaonekana pia
amefanya masomo ya biashara kinyume cha
utaratibu na sheria za mitihani.
Alisema mwanafunzi Habib Ibrahim naye alifanya
mtihani huo wa Taifa, lakini katika matokeo hayo
inaonyesha kama hakufanya mtihani huo, jambo
ambalo sio la kweli.
“Kutokana na utata huu, hatuwezi kukubaliana
kabisa na matokeo yaliyotangazwa na kwamba
kuna haja ya Wizara ya Elimu kuingilia kati jambo
hili haraka, ili haki itendeke kwa kila mmoja.
“Kwa matokeo haya, ni hakika hawakutenda haki
na mfumo wao mpya wa kusahihisha mitihani
kwa kutumia namba pekee umehujumiwa.
“Tunataka usahihishaji wa matokeo ya wanafunzi
wetu urudiwe upya. Kwani hali hii imewafanya
wanafunzi wengi kuathirika kisaikolojia kwa
matokeo haya ya uongo yaliyotolewa na NECTA,”
alisema Bujugo.
Hali hiyo imezua taharuki kwa wanafunzi wa
shule ya Green Acres, jambo lililowafanya baadhi
ya wazazi kulazimika kufika shuleni hapo na
kupanga kuitisha kikao cha dharura Jumapili
ijayo ili kujadili hali hiyo.
“Jumapili wazazi watakutana hapa shuleni kwa
ajili ya kujadili hali hii na hata kutokana na
uchambuzi wa matokeo ambayo bado
yanaendelea kuchambuliwa, ninatumai mambo
mengi tutayabani kutokana na uchakachuaji huu
wa matokeo ya wanafunzi wa shule yetu.
“Katika hili nipo pamoja na wazazi na kubwa
tunabaki na msimamo wetu wa kutaka ni lazima
usahihishaji urudiwe na kwa gharama za baraza
lenyewe. Huu ni ukandamizaji na uchakachuaji
wa wazi ambapo haulipeleki Taifa letu pazuri,”
alisema.
Hata hivyo MTANZANIA ilipomtafuta Ofisa Habari
na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi, alitaka
apewe muda wa dakika 30 ili kuweza kupata
ufafanuzi wa jambo hilo kwa kina.
Baada ya muda huo, Nchimbi aliwasiliana na
MTANZANIA na kusema kuwa hakuna kitu kama
hicho, kwani NECTA imekuwa makini katika
mfumo wa usahihishaji na madai ya shule hiyo
hayana ukweli wowote.
“Swali moja katika mtihani husahihishwa na
mwalimu mmoja, sasa inawezekana vipi kwa mtu
ambaye hakufanya mtihani apewe maksi, hili
halipo na hata ukiangalia mtandao wa NECTA
umeweka wazi kila kitu,” alisema Nchimbi.
Katika matokeo hayo ya kidato cha nne
yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru
Kawambwa, zaidi ya asilimia 60 ya watahiniwa
wamefeli.
 
hizo 60% zinaanzia kwa wale wanaenda kidato cha kwanza bila sifa...
 
Daaaaa! u tra tra mtupu! naomba nyie wenye tabia yaku i review habari nzima hlf ndo mnacomment muache mna2chosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…