Matokeo kidato cha nne batili

PCGAMES

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
782
Reaction score
1,157
Kweli alieshiba amjui mwenye njaa. Matokeo ya mwaka jana ni batili coz huwe ukapandisha alama za wahusika bila kumjulisha au kumtaalifu muhusika mwenyewe, kuanzia wanafunzi, walimu, wazazi na wananchi wote kiujumla. Hizo alama za juu za 4m 4 kiukweli zimewaumiza wanafunzi wengi kiasi kwamba hadi wengine wamepoteza maisha yao kwa uchungu, hadi mwanafunzi kuamua kupoteza maisha yake inamaana hizo hazikuwa alama alizostaili kupata na ikumbukwe kuwa kabla ya mitihani ya kitaifa huwa na maandalizi kama vile mitihani ya moko na mingineyo sasa huko kote matoke yalikuwa ya kawaida then uje kupata matokeo mabaya ghafla kisa mijitu michache imekaa wao wenyewe na kujipangia kwa manufaa yao wenyewe sasa hii ni haki kweli? Hakukuwa na maandalizi yoyote kwa watahiniwa wala taarifa yoyote kuhusu kupandishwa kwa alama za mitihani sasa huoni kuwa haki haijafanywa hapo kwa wahusika? Mtahiniwa anafanya mtihani darasani huku kichwani kwake akiwa na mbinu ya kuvuka alama za ufaulu zilizo zoeleka alafu yanatoka majibu yake mabovu, wewe unafikiri atachukua uamuzi gani na ukizingatia anauwakika wa kufaulu coz kwake yeye kufaulu sio kitu kigeni. Alafu baadae unakuja kuambiwa alama zimepandishwa. Jamani kwa upeo wangu hii haijakaa sawa na Necta hawawezi kukubali kirahisi kushusha hizo alama coz lazima baadae itajitokeza hoja ya kuwataka wao wajieleze kwa nini walipandisha alama bila taarifa kwa wahusika? Na ukizingatia kuna wanafunzi wamepoteza maisha kwa ujinga au upuuzi wa watu wachache. Fikiria unafikiri nini kitaendelea hapo? Na hilo ni suala moja tu, kuna mambo mengi nayo yaliyochangia matokeo kuwa mabaya mojawapo ni usahihishaji mbovu wa hiyo mitihani so yote hayo Necta watatakiwa kujieleza. Necta pale kuna mapungufu makubwa miaka kibao ila hawezi kujishtaki wenyewe badala yake watajisafisha kwa njia yoyote ile, moja wapo ni hilo la upangwaji upya wa matokeo. Tusipende kushobokea vitu tusivyovijua au kuvifahamu kikamilifu kwa sababu kuna watu wanalaumu utadhani anauhakika na anachokifikiria akilini mwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…