Matokeo makubwa kwa wakulima wa nyanya Tanzania

Dawa za kuzuia wadudu zinazotumika.... Zina madhara gani kwa sisi watumiaji?? Interval ya kupuliza dawa na kuvuna ikoje??
Dawa nyingi zinazotumiwa katika shughuli za kilimo nchini ni lazima zithibitishwe na taasisi ya utafiti wa viuatilifu(TPRI) iliyopo Arusha.
Kwa ufupi ni kwamba kila kitu kikizidi au kutumiwa vibaya kina madhara, label ya dawa ni lazima iwe na maelezo sahihi na ya kutosha ili kuepuka madhara si kwa mtumiaji wa mwisho pekee bali na kwa mkulima mwenyewe anayehusika na upuliziaji wa viuatilifu hivyo.
Tatizo kubwa ambalo binafsi nalishuhudia kila siku ni kwamba wakulima wengi kwa kutokujua hawazingatii matumizi sahihi ya viuatilifu. Mambo ya ku-overdose(hasa dawa inapogoma kutibu mimea), kutovaa mavazi ya kujikinga, kutozingatia muda wa kupuliza dawa na kuingia shambani au kuchuma n.k, ni kawaida sana mashambani na hasa kwa mazao ya mboga mboga.
 
vp unaonaje mkuu ukianzish group la whatsap tuendelee kujifunz zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombeni kujua ni booster gani ya matunda nu nzuri, nyanya yangu imefikia hatua hii, pia naomba kujua dawa nzuri ya kuua wadudu wa kantangaze
 

Attachments

  • Screenshot_20220918-193359_1.jpg
    57.3 KB · Views: 34
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…