Matokeo Mapya ya Kidato cha 4 mwaka 2012 Yanaliaibisha Taifa Letu

Joined
Jan 19, 2013
Posts
23
Reaction score
21
Wenzangu wana JF,

Ninaelewa kwamba hakuna taifa lolote lililoendelea duniani pasipo kuimarika kwa elimu. Nimeyapitia kwa haraka haraka matokeo yaliyotangazwa jana na nimegundua matatizo ambayo ni "irreparable" yanayofanya waziri na manaibu wake wawajibike kisiasa kwa kushindwa kazi. Mfano mdogo ni mtahiniwa huyu hapa chini. Kwa jinsi matokeo na uhalisia wa matokeo yake, angepaswa kuwa na Daraja la 4 na Alama 33 (Div 4 Points 33). Badala yake angalieni kinachoonekana sasa. tatizo hili naamini alipo kwa huyu mmoja tu. Tunaipeleka wapi nchi yetu kwa siasa zetu hizi za kuchezea matokeo ya watu wetu?

[TD="width: 6%"] S3735/0072
[/TD]
[TD="width: 4%"] M
[/TD]
[TD="width: 6%"] 32
[/TD]
[TD="width: 4%"] IV
[/TD]
[TD="width: 58%"] CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F PHY-F CHEM-D BIO-D B/MATH-F
[/TD]
 
Mleta maada wewe ndo umefeli kwa hili japokuwa siisapoti salikali kwa mabaya mengine ni hivi, masomo 7 ndiyo huwa yanatumika kupata pointi na ni yale ambayo mtahiniwa amepata gredi zuri zaidi. Kwa mjibu wa huyu mtahiniwa ana D=3 na F=4 jumla itakuwa masomo saba kama nilivyosema. Hivyo basi point hizo zitakujumlishwa kama ifuatavyo
D=4 points
F=5 points
3x4 + 5x4 = 32 (Division four with 32 points) Balaza wapo sahihi
 
Tz nchi yangu..........
Maajabu saba ya Dunia.
 

D zipo 3
F zipo 6
Jaribu kutumia miwani unaweza ukaja na kitu hapo.
 
taifa la manunda, hakika hii ni ajabu ya dunia, ina maana watanzania hatuna uwezo mpaka tusaidiwe?? tunawajengea watoto wetu utamaduni gani?? aibu ya dunia
 
Mtoa mada umeteleza. NECTA haiwezi kufanya koso hilo. Hata watoto wa Form 3 ambao ni committed hawawezi kushindwa kupanga Div na pts zake. Ni bora ungeuliza kuliko kuitupia lawama serikali. Bahati nzuri jamaa wa JF wamekupatia formula nzuri ya kupata Div na points zake.
 

Mkuu, kumbuka kupata Div na Points NECTA wanachukua masomo 7 uliyofaulu vizuri plus masoma ya Lazima pia yanachukuliwa. Masomo ya Lazima kwa O'Level ni Math, English.

Huyu Mwanafunzi ana D tatu (3*4=12) na F chukua 4 (4*5=20). Jumla ana Div IV ya Point 32.

Mkuu, revisit vizuri jinsi ya kupata hii makitu. Kama hujaelewa reply back nitakugongea tena mahesabu, ha ha ha ha !
 
Du nina kazi kwelikweli!!!! Nimesema pointi huwazinahesabiwa kwa kutomia masomo saba tu! na si vinginevyo. Hakika wewe hujamaliza form four.

Mkuu, humu ndani sijui hawa watu wanaoleta mada wamemaliza kweli Form Four au Six?? Mbona hili linajulikana, kuwa ni Masomo 7 ndo yanachukuliwa? Kweli humu mkuu kuna kazi katika masuala ya Elimu!
 
Hilo ni tatizo la kuleta mambo jamvini kwa jazba. Ni vema kutulia kidogo kabla ku post mambo humu maana mwisho wa siku unajikuta una expose ignorance yako
 

Mkuu matokeo haya yako sahihi. Katika kuweka alama wanachukua masomo saba tu uliyofanya vizuri katika masomo yote uliyojiandaikishia mtihani. Kwa mfano candidate huyu ana masomo 9 kwa hiyo wanachuku D tatu alizofauli kila moja point 4 kwa hiyo jumla points 12. Wanachukua F 4 kila moja point 5 jumla points 20. Jumlisha 20 na 12 unapata jumla ya points 32. Pole kwa kusahau utaratibu.
 
mambo haya wizara ilitakiwa kuyafanya kitambo ndani kwa ndani kabla ya kutapika hadharani
 

Pia mwambie haya matokeo yanatoka automatically. Yaani wameset system wana sheet ambayo ukiweka alama ulizopata zinaenda dondoka kwa sheet nyingine ambayo inaweka grade A-F kulingana na maks range walizoweka kwa hiyo makosa hayapo labda iwe katika kuingiza maana katika computer systeme cabbage in= cabbage out.
 
ukistaajabu ya mirembe, utaona ya TZ. hiyo ndiyo TZ zaidi ya uijuavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…