Kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu kwa kupunguza alama za ufaulu ni kosa kubwa. Kwa kuwa tumeruhusu wanafunzi wasio na uwezo kwenda sekondari, ndio hao hao watakaosababisha zoezi kama hili kuendelea kidato cha pili, baadae kidato cha nne. Si ajabu kidato cha sita na vyuo vikuu. Ili elimu ipande inatakIwa kuwe na ushindani kufaulu kuanzia darasa la saba.
Miaka ya nyuma wakati shule za sekondari zilipokuwa chache kulikuwa na ushindani mkubwa kwa wanafunzi na walimu katika kuingia sekondari, ndio maana waliotutangulia wana uwezo mkubwa kulinganisha na wanafunzi wa sasa, na bado tunajidai elimu inakua, kwa kupeleka wastani wa alama 20 sekondari? SHAME.. Enzi hizo huna wastani wa alama 70 sekondari utaisikia redioni labda unde shule za binafsi, na ilikuwa inaeleweka kabisa waliosomea shule za binafsi ni wale waliofeli darasa la saba (Ukiacha shule za Agakhan-Wahindi na seminary) sasa hivi kinyume. Inasikitisha na sijui tunaipeleka wapi nchi hii. Tusubiri mikataba mibovu, uchumi mbovu, uongozi mbovu yaani kila kitu kitakuwa kibovu.
Maoni yangu ni kwamba ufanyike utafiti kujua nini kifanyike katika kuboresha elimu, bila kuwahusisha watumishi wa wizara ya elimu. Tuache siasa za eti elimu imekua kwa kupeleka watoto wengi sekondari zisizo na ubora. Afadhali kuwa na shule chache zilizo bora kuliko kuwa na shule kila kata zisizo na elimu bora.