Matokeo ya darasa la 7 ni kituko na ni aibu!

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Posts
409
Reaction score
135
Wanajamvi fikra huru.
tunakazana kuhamasishwa Mlima kilimanjaro uingie kwenye majabu ya dunia badala ya kuingiza matokeo ya darasa la saba ambapo wamefanya mtihani wa masomo 5 Waziri katangaza wenye D daraja lenye maksi 50 mpaka 100 nao wamefauli hiyo ina maana waliopata 10 mpaka 20 kwa kila somo mwaka huu wamefaulu. Wakati mwaka jana wenye jumla ya alama 150 waliochaguliwa 5200 iligundulika na Mulugo Strategy hawajui kusoma na kuandika je hawa wa alama 50 ndio itakuwa maajabu huko sekondari.
Siasa za Tanzania zinaiweka elimu yetu kuwa na sifa za kuingizwa kwenye MAAJABU ya Dunia na hii na kutokana na Elimu kuongozwa na siasa badala Elimu kuiongoza Siasa ukitaka kugundua hilo angalia watalamu mpaka wenye phd, Prof. na Wanasiasa nani anapewa nafasi kwenye mamuzi muhimu kama ya elimu.
Wanajamvi Vp tukaona umuhimu wa kupigia KURA Matokeo ya Darasa la 7 kuingizwa kwenye Maajabu ya Dunia badala ya Mt Kilimanjaro maana Kiwango cha ufaulu kwa miaka 7 na mwaka huu imelazimu Kuambiwa wenye JUMLA ya 50 wamefaulu
 
[h=3][/h]

[h=5]MCHAMBUZI: IMORI
MARK
[/h]
[h=5]MATOKEO YA DARASA LA 7 NI KITUKO NA NI
AIBU KWA TAIFA TOFAUTI NA ILIVYOWAKILIWASHWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA WAZIRI
HUSIKA.
[/h]
[h=5]WAZIRI ALISEMA IDADI YA WALIOENDA
SEKONDARI IMEONGEZEKA UKILINGANISHA NA MWAKA JANA LAKINI JE WAJUA UFAULU
WAO???
[/h]
[h=5]------------------------------------------------------------------

WALIOPATA:
A - 3,087,
B - 40,683,
C -
222,103
CHUKUA A+B+C = 265,873


WALIOCHAGULIWA KWENDA KIDATO CHA KWANZA NI
560,706.
[/h]
[h=5]
KWA HIYO WATAHINIWA
294,833 WAMECHAGULIWA KUTOKA DARAJA "D"
.......WAKATI DARAJA LA UFAULU KWENDA SEKONDARI NI KUANZIA "C"
....
YAANI ALAMA 101/250.

ZAIDI YA 51% YA
WALIOCHAGULIWA NI KUTOKA DARAJA "D" YAAN CHINI YA ALAMA 100/250.

JE, KTK HAWA 294,833 TUTAKOSA WASIOJUA KUSOMA NA
KUANDIKA VIZURI?
[/h]
 

Sisi kweli hatujirekebishi kutokana na makosa,Tunajali zaidi siasa,tena kuogopa kelele za wananchi.
Sasa Mtihani wa Form TWO,matokeo yatakuaje,mtihani wa Form Four si itakuwa balaa nyingine.Kitu cha ajabu wanasiasa hao hao watasema kwanini wanafunzi wamefeli mtihani wa FORM FOUR,na itaundwa Tume kuchunguza sababu za kufeli.

Serikali isikwepe ukweli,kushusha kiwango cha alama za ufaulu sio kuwasaidia wanafunzi na wazazi bali ni kujenga Taifa la wajinga,wavivu na janga lingine la Taifa.Yaani kizazi kijacho kitakuwa na wanafunzi DIVISION ZERO nyingi sana.

Mbona siku za nyuma wanafunzi walifaulu wachache na hapakuwa na kelele,kwani waliochaguliwa walikuwa ni wanafunzi ambao hata jamii ilikubali kuwa ni wanafunzi wenye uwezo na shule walizokwenda kusoma ziliheshimika.Sasa mbona tunarudi nyuma.Hata vitabu vya kusoma madarasani Wizara imebinafsisha{ukienda mkoa tofauti wanasoma vitabu tofauti},kweli Wizara yenyewe imejichanganya,bado inatakiwa kujipanga upya.

Zama hizi za utandawazi sisi kama Taifa ndio tunafanya Ujinga kuzorotesha Elimu yetu,tutakuwa na kizazi chenye kulalamika kila siku.
 
Viongozi husika wameamua hayo yote (kudumaza elimu Tanzania)
 
Hii nayo kali ya mwaka,sasa wizara ya elimu inatakiwe ichunguzwe.
 
Siku ya kwanza kufika darasani baada ya kupewa vipindi niliuliza form 1 wote swali dogo tu tena kwa kiswahili. Jee tunaishi nje au ndani ya dunia? Kati ya watoto 154 ni19 tu walisema tunaishi nje na wengine waliobaki. walisema tuko ndani. Tafakari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…