Matokeo ya form four 2012 - Je na Teknolojia ya mawasiliano imeangaliwa??

Destin

Member
Joined
Dec 5, 2012
Posts
12
Reaction score
2
Wanasema kila jambo lina uzuri na ubaya wake...hivi karibuni tu Taifa la Tanzania limepokea matokeo ya form four ya mwaka 2012. Matokeo yanaweza kuwa mazuri au mabaya,kwenye hili tunazungumzia matokeo mabaya na ya kutisha ambayo hayajawahi tokea kwa kipindi cha mwaka 2000 mpaka kipindi hiki ya yaliyotokea.Hii ni kwa mujibu wa Katibu wa wizara ya elimu Joyce Ndalichako.

Yapo mengi yanayoonyesha kusababisha matokeo haya mabaya kulingana na maono tofauti ya watanzania. Kuna hili la teknolojia ya mawasiliano....Je hili nalo si sababu?

Wanafunzi wengi wa kisasa wamekuwa wakimiliki simu za mikononi,tena wengi wao hupewa simu hizi na wazazi wao kwenye level ya primary na secondary,wazazi wamekuwa wakifanya haya kwa kisingizio cha mawasiliano na wanao pasipo kuelewa madhara yake,inawezekana pia wakawa wamefanya ili mradi tu kuwaweka watoto wao katika mfumo wa kisasa. Binafsi naliona hili ni tatizo,tena si dogo. Watoto au wanafunzi hawa wamekuwa wakiutumia muda mwingi sana katika teknolojia ya mawasiliano,tena si mawasiliano ya kujenga bali ya kubomoa. Unakuta mwanafunzi badala ya kutumia vitu kama google kupata "constructive information"....badala yake unakuta anatumia muda mwingi ku-chat kupitia Facebook,Twitter,Whatsapp na kadhalika. Wakati mwingi kuingia kwenye blogs za mapenzi hasa zile chafu n.k

Wanafunzi unakuta saa 6 za usiku wana-chat kwa kutumia zile offer za makampuni ya simu,tena wakati mwingine wanafanya hivi na unakuta kesho yake wana mtihani wa majaribio au mtihani kabisa.

JE HILI LA KUWAACHA WANAFUNZI KUMILIKI SIMU KATIKA HATUA ZA AWALI HALIWEZI KUWA NI KIDONDA KIKUBWA TU ?
 
Umeeleza vizuri uzuri wa technologia kumbe tatizo ni matumizi mabaya ya technolgia, ila je hao wanaowapa hizo simu huwa ni kwa mdhumini gani maana nilitegema ndio wangekuwa wakwanza kudhibiti haya matumizi ambayo mimi na wewe tunayaona sio sahihi
 
Back
Top Bottom