Matokeo ya Kenya yatangazwa (KCSE) linganisha na Tanzania (CSEE)

Na vile vile hakuna Form VI. Sasa mnalinganisha Sukari na Chumvi?

Umeona ehee, Hawa Jamaa kuanzia aliyeleta mada mpaka wanaoshabikia humu ni weupe Kichwani, ni kama mimi niende sijui Togo, nije hapa niwaletee matokeo ya Mtihani wa Togo na kuwaambia angalia wenzetu wanavyofaulisha bila kujua kwamba Togo na TZ tuna mifumo miwili tofauti kama ilivyo Kenya na Tz! Huwezi kulinganisha vitu visivyolingana!

 
Mkuu ni wapi tulipolinganisha matokeo ya form IV na form VI? Hapa tunazungumzia KCSE na CSEE. Kwa maana hiyo matokeo tunayozungumzia hapa ni yale yale ya kidato cha nne kwa pande zote. Sasa hebu niambie kama na sisi tungekuwa tunawapeleka chuo kikuu moja kwa moja hao wanaomaliza form IV mwaka huu ungekuwaje?

Ukweli ubaki pale pale kwamba sera yetu ya elimu inahitaji marekebisho makubwa sana. Na hawa mawaziri uchwara wanaopewa hizi wizara kwa kufuata ujomba hawatatutoa!! Bado tunachechemea hatujui tuende wapi!
 

Tukiweka hapa mtihani wa Physics wa KCSE na Physics ya CSEE ndio utanielewa na maaanisha nini, We endelea tu kujidharau.
 
sisi wizara yetu changamoto ya kwanza ni kutopata mawaziri wenye elimu wanaoongoza wizara nyeti ya elimu.

hebu nikumbushe muungano wa Tanzania ni Zimbabwe na nini vile??
 
sisi wizara yetu changamoto ya kwanza ni kutopata mawaziri wenye elimu wanaoongoza wizara nyeti ya elimu.

Hilo neno nalichukia sana siku hizi. Linatumika kuficha udhaifu wa viongozi wetu! Badala ya kukubali kwamba kuna uzembe, wao wanaia changamoto
 
Hilo neno nalichukia sana siku hizi. Linatumika kuficha udhaifu wa viongozi wetu! Badala ya kukubali kwamba kuna uzembe, wao wanaia changamoto
uzembe ndo changamoto yenyewe, au wewe mwenzetu unaelewaje hilo neno?
 
uzembe ndo changamoto yenyewe, au wewe mwenzetu unaelewaje hilo neno?

Vyovyote vile...But I hate it. Yaani imeshakuwa tabu, tangu jamaa wazembe wazembe wa serikalini, waligundue hilo...Imekuwa tabu
 

Nimeona niweke vizuri hapo kwenye red kwaajili ya record, otherwise tuko pamoja.
 
Ndiyo maana wakijenga reli sisi tunajenga mfereji. Wakijenga highway, sisi tunajenga vichochoro. Kisa? Elimu ndogo!


wanajenga flyover sisi huku wakandarasi wabomoe daraja chini ya kiwango yakikamilika yanapewa jina la kitaifa Dr.Kj
 
Tanzania kujilinganisha na Kenya kielimu na uchapakazi ni sawa na kusema maji ya mfereji=maji ya bahari!! Na EAC watatutawala na kuchukua kazi zote!! Eti mnajidai kuwa na Federation!!! Mpaka Burundi na DRC watatushinda kama hatutakuwa makini.
 
Mbona naona Siasa tu hapo. Hakuna Takwimu za maana. Wangapi wamepata Div I, II,III ??. Sijaona kitu kinachokushangaza.

Mkuu kule kwao hawana Div wana mean grade yaani A,-A,+B,B,-B,+C,C,-C na kuendelea mpaka E.
 
Tukiweka hapa mtihani wa Physics wa KCSE na Physics ya CSEE ndio utanielewa na maaanisha nini, We endelea tu kujidharau.
Naona wewe sasa unataka kudandia treni kwa mbele!!

Mimi nina ushahidi wa mtu aliyetoka KCSE (akiwa amepata B+) na kuja kusoma TZ (yeye ni m-TZ) ACSEE na alichokifanya ni hatari tupu! Juzi ka-graduate Bugando kama MD maana alikuja kusoma PCB hapa Tz. Kilichofanyika kule Kenya hakuwa amefanya mtihani wa Biology, hivyo alipokuja hapa alitakiwa kurudia mtihani wa Biology ya TZ na akafaulu. Sasa unapotuambia Physics ya Kenya na Tz ni tofauti sikuelewi!!

Kazi ni kwa Kawambwa na Mulugo (Mzee wa Zimbabwe!!)
 
Kenya wanajua wanakotaka kwenda na viongozi wao wako fucused kulifikisha taifa lao huko; tofauti na sisi hapa ambapo viongozi wetu are more focused kwenye kuchumia matumbo!

Tumebaki kuwa taifa lisilo na vision wala mission tunapwaga mbuga bila kutambua tunakotaka kuelekea!!

Elimu ndio ufunguo wa maendeleo; sio Kilimo kwanza na matrekta feki; power tillers!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tume ya Pinda iende Kenya baada ya uchaguzi mkuu wakapigwe darasa; au wamualike Mutula kilonzo waziri wa Elimu wa Kenya aje ampe tuisheni Shukuru Kawambwa na udaktari wake wote anafanya mabo ya aibu tupu!!
 
Wewe watu wanasoma kule acha huku tunatafuta C tatu.elimu ina wadau wengi wanaotekeleza their professional duties sio ushemeji
Hayo matokeo ni ya kisiasa zaidi la yamelenga kutokuchafua hali ya hewa kipindi hiki cha uchaguzi.uwe mbunifu na mfuatiliaji wa mambo hebu wamletee ndalichako ayasahihishe upya uone shuguli ya jeshi
 

Kwa hili la hao Vilaza wawili nakuunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…