Matokeo ya kidato cha II yamechakachuliwa

magistergtz

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
282
Reaction score
56
Ktk kipindi cha Jenerali ulimwengu cha channel ten cha leo tarehe 25 January, imebainishwa matokeo ya kidato cha 2 hayakuwa halisi. Takwimu zilipindishwa kuushawishi umma kuwa kiwango cha elimu ni kizuri. Takwimu hizi za ufaulu wa 65% ni uongo kwa vile hauendani na tafiti nyingine, mfano za Twaweza. Lkn pia watoto hawa tunao na tunaishi nao, hawajui hata kusoma wala kuandika wengine. Asilimia zaidi ya 90 ya watoto hawa hawawezi kusoma wala kuandika kiingereza. Wamefauluje mitihani ilofanyika kwa kiingereza?

Ushauri: Wizara ya elimu acheni siasa ktk takwimu za elimu. Tuache watanzania tujue ukweli wa uwezo wa watoto wetu
 
Tatizo si utoaji wa takwimu batili bali swala ni; chanzo cha wao kutofanya vizuri ni nini?
 
Moja ya shule ninazozifahamu matokeo yamekuwa kama ifuatavyo Mwanzi sekondari watahiniwa walikuwa 144 WALIOFAULU ni 6 sawa na asilimia 4.2. MANYONI SEKONDARI watahiniwa 126 waliofaulu wanafunzi 4 sawa na asilimia 3.3 sasa hata kama kuna buffering ya kutosha kutoka shule za binafsi hatufikii hapo 65.
 
mkuu cjui cjakuelewa ama nimeshindwa kuamini maana kama wamefaulu 6 hao waliobaki 138 wamefeli ama inakuwa je?
 
Habari za uhakiki kutoka ofisi za Ukaguzi ambao ndiyo wanaoshughulikia Mtihani wa Kidato cha Pili zimethibitisha kuwa waliagizwa waongeze alama 12 kwa kila somo kwa watahiniwa ambao walikuwa wamefeli. Hii inamaana kuwa mtahiniwa aliyekuwa na wastani wa alama 18 ameonekana kuwa amefaulu mtihani kwa kuwa walipewa alama za bure 12 kila mwanafunzi kwa kila somo? Hili linawezwa kuthibitishwa kwa kuangalia karasasi za majibu ya wanafunzi na kulinganisha na matokeo yao yaliyotangazwa.

Kwa hali hiyo wakuu tutegemee nini kwenye upatikanaji wa nguvu kazi ya taifa kwa siku zijazo? Hivi kwa nini wasingeacha matokeo kama yalivyo na kutafuta sababu kwa nini yamekuwa mabaya kisha wachukue hatua stahiki? Je kinapotangazwa ktu cha uongo, hatuoni kuwa ndiyo tunazidi kudidimiza taifa kwa sababu wahusika wakisikia matokeo ya kuchakachuliwa yametangazwa wameambiwa kiwango chao cha ufaulu kimeongezeka wanapumzika raha mustarhe na kujipongeza wakati hali halisi ni mbaya sana. Nina imani kama matokeo hayo yangetangazwa bila kuchakachua, jamii ingetaka walimu na serikali kwa ujumla iwajibike zaidi na huenda huo ungekuwa ndiyo mwanzo wa kupata suluhu ya kudumu ya kuboresha mfumo wa elimu.

Kwa kweli hali inasikitisha, tufanyeje ili kujikwamua????
 
sasa kama kuna mtu kapata alama 90 akiongewa 12 si atapata mia na mbili,inakuwaje hapo
 
Yaani wao mameongeza alama bila kujali hilo. Waliokuwa wanapata zaidi ya 100 baada ya kugawiwa alama 12. za bure kwa kila somo wamepewa 100. Lemgo kuu ilikuwa mi kusaidia walio wengi ambao alama zao zilikuwa chini sana. fikiria hata baada ya kupewa alama 12 za bure bado waliofeli ni laki 135
 
sasa kama kuna mtu kapata alama 90 akiongewa 12 si atapata mia na mbili,inakuwaje hapo

mbona unakuwa na kichwa kiGumu cha kuelewa jamaa kasema wastan wa 12 uliongezwa kwa wale waliofeli tu
 
Back
Top Bottom