Umenena jambo ambalo kwa siku nyingi linanikera sana. Naona kwamba kuna watu kazi yao ni kupanga mipango ya kuwamaliza tu Watanzania. Yaani mwanafunzi anakamuliwa shilingi 20000/= Halafu bajeti inasema trilioni moja kwenye elimu. Ukitaka kuona matokeo yako utoe fedha. Huu ni unyonyaji wa wazi kabisa, Watanzania tunadharauliwa sana.
Tukumbuke Dr Mwl Nyerere alisema, "Mtu anayekuheshimu, akikwambia kitu cha kipumbavu, halafu ukakubali anakudharau." Pia alisema, "Unamwonesha mtu dhahabu, halafu yeye anakuonesha kichupa chenye rangi ya dhahabu, halafu anasema, 'Hii ya kwako siyo dhahabu, lete hiyo nikupe hii ya kwangu,' unampa halafu unaanza kukenuka kama Zuzu ni ujinga mkubwa."
Maneno haya yaliyosemwa na Dr Mwl Nyerere ndo msingi unaotumika kuwapatia kula mafisadi. Wanaelewa we are not rational. We don't integrate things, we think upside down. Hata kama wakijenga illogical premises sisi tutakubali tu.
Jamani basi tuwe na akili. Mara watoe matokeo kama siri, mara wachelewe kutoa matokeo, mara mitihani iibiwe, nk....... Yote haya hayatufanyi tuamke?