Matokeo ya kidato cha nne, AIBU KUBWA KWA CLOUDS FM, PJ, Gerald Hando, Kibonde na Wasiwasi

understanding

Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
75
Reaction score
34
Naombeni msikilize ujinga wa Clouds Fm, nime tune clouds Fm, nilitegemea kusikia leo watangazaji wangekuwa wakali sana kuhusu kufeli kwa watoto wa kidato cha nne kama walivyokuwa wakali wakishadadia kusitishwa kurushwa kwa bunge live na spika kuzima hoja ya Mbatia. hawa watu hawana aibu hata kidogo na wala hawajui nini kinaendelea.. nazidi kuuliza, how ethical these people are? yaani hapa namsikia Kibonde na wasiwasi wakitoa sababu za kufeli kwa wanafunzi, HAKUNA hata mmoja anayemponda au ku-comment negative kuhusu waziri au kuteteas point ya Mh Mbatia?

Narudia tena, ebu angalie ujinga wa PJ na Gerald Hando, walishadadia sana wiki iliyopita kuwa wabunge wanatoa hoja na wanakuwa wakali ili kujishaua, tena wakashadadia sana spika kuzima hoja ya Mh Mbatia, sasa aibu gani hii? hivi wanajisikiaje wajinga hawa kuona matokeo ya watoto yako yalivyo??

Narudia tena kuwaomba elimu zao na vipato vyao, kuna sababu kubwa wao kufanya hivi, ni njaa? ni ujinga? ni kujikomba komba? Ni kulogwa? ni nini haswa???... waandishi gani hawa?? penye kuhitaji kupiga kelele wanakuwa kimya, kwenye kuhitaji kimya na busara wanapiga kelele.. wapi na wapi?
 
Hivi ni mwaka gani ambapo matokeo ya shule za sekondari yalikuwa mazuri saaana?
 
Ndio umeandika nini sasa! Unadhani kila mtu huwa anasikiliza redio?
 
Walimu migomo,je tutapata wanafunzi hodari kweli?
 
Huyo Kibonde form IV alipiga ZIRO pale Mzizima....kwahiyo usishangae sana
 
Hivi ni mwaka gani ambapo matokeo ya shule za sekondari yalikuwa mazuri saaana?

Matokeo mazuri ni yale yenye kutengeneza normal distribution curve. Ambapo watu wengi uwa wapo katika kiwango cha ufaulu wa kati, na wachache kwenye viwango vya ufaulu wa juu sana na chini sana.

Sasa katika siku za hivi karibuni, distribution curve imekuwa very skewed, kukiwa na rundo la wanafunzi waliofeli sana kuliko waliofaulu kwa kiwango cha wastani na cha juu zaidi.

Sina kumbukumbu kama kuna kipindi kiwango cha ufaulu wa juu sana kilizidi ufaulu wa wastani na wa chini sana. Hii nayo utengeneza skewed distribution curve.
 
Hivi ni mwaka gani ambapo matokeo ya shule za sekondari yalikuwa mazuri saaana?

...mkuu, ni mwaka uleee kabla hatujapeleka wasiojua kusoma sekondari...kabla elimu haijawa siasa...wakati ule tukiwa na shule chache zenye kujua kazi yake...ndio wakati ule kabla ya kuwaambia wanetu "mnafelishwa na mfumo flani"...wakati ule kabla elimu haijawa biashara....wakati ule walimu wakiwa na "wito"...wakati vitabu vya kufundishia vikiwa vinafanana kwa nchi nzima....wakati wazazi wakizingatia elimu ya vijana wao...kabla ya biashara ya "feki" haijakolea....
 
Sina kumbukumbu kama kuna kipindi kiwango cha ufaulu wa juu sana kilizidi ufaulu wa wastani na wa chini sana. Hii nayo utengeneza skewed distribution curve.

Hilo walau ndo jaribio la jibu la swali langu.

Je, kuna mwaka ambao matokeo ya hii mitihani ya taifa yalipokelewa kwa furaha kwa sababu ya ufaulu mzuri wa watahiniwa?
 

Huo wakati hauna mwaka au miaka?
 
Kibonde alitaga form 4! Matokeo yake yalibandikwa mwenge stand
 
Hilo walau ndo jaribio la jibu la swali langu.

Je, kuna mwaka ambao matokeo ya hii mitihani ya taifa yalipokelewa kwa furaha kwa sababu ya ufaulu mzuri wa watahiniwa?

Hapo inabidi kupekua makabrasha ya historia ya matokeo ya sekondari, ili kupata jibu la uhakika.

Kwani katika kumbukumbu zangu za harakaharaka, sijawahi kusikia hilo.
 

km cjaona point za hao watu uliowataja zaid ya kuona tu maneno yko.....
 
Hivi ni mwaka gani ambapo matokeo ya shule za sekondari yalikuwa mazuri saaana?

Chifu, Kitila ametoka uchambuzi juu ya athari za matokeo haya kwa vyuo vikuu. Ametuma kwenye group la Wanazuoni.

Katika uchambuzi huo ametoa kidogo historia ya ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne toka mwaka 2000.

Naamini utapata jawabu lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…