JOSEPHAT J BAZA
Member
- May 4, 2013
- 27
- 22
Nathubutu kusema kuwa matokeo ya kidato cha 4 yaliyotangazwa awali na NECTA kupitia kwa waziri wa elimu Dk. Kawambwa ndiyo matokeo sahihi kwa wanaopenda maendeleo ya elimu hapa nchini. Uchakachuaji huu unaoandaliwa na serikali kwanza ni kuvunja sheria ya NECTA kwa lengo la kujisafisha kisiasa. Watanzania wote wanaopenda maendeleo ya elimu nchini waipuuze kauli ya serikali ya kutaka matokeo haya yachakachuliwe upya. Ni bora kupata wanafunzi wachache bora kuliko kupata maelfu feki. Serikali inafaa kufikiri kwa kina kabla ya kukurupuka kufanya maamuzi yasiyo na tija kwa mustakabari wa elimu hapa nchini.