Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 482
Hahahahahahhahahahahaha! hii imeniacha hoi, Mkuu Ngaramtoni Standing allowance inakuwaje na hulipwa kwa kuangalia vigezo vipi, mwalimu afundishae akiwa amekaa anastahiki hii kitu?
Hivi matokeo ya kidato cha pili hupatikana wapi? Shuleni ama nayo huwekwa mtandaoni? There is a member of my family dying to study science! The issue is shule anayosoama haina waalimu wazuri wa masomo ya science. Kwa muodoko huu mnaonambia kuwa wanafunzi wa kidato cha pili wame-fail naona jinsi ndoto yake inavyoyeyuka!
Hayawekwi mtandaoni, yanapatikana katika ofisi za ukaguzi Elimu Kanda, Baada ya kutoka yanakuwepo shuleni kwa Mkuu wa Shule au Ofisi ya Taaluma. Matokeo bado hayajatoka ila karibuni hapa yatakuwa tayari. Si wote waliofeli wapo walifanya vizuri, huenda huyo wa kwako amefanya vizuri.
Kuna taarifa kutoka kwa wasahihishaji wa mtihani wa kidato cha pili wa mwaka 2012 kuwa HALI NI MBAYA SANA na kuna shule huenda zikakosa kabisa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tatu kwa mwaka 2013! Taarifa zinaeleza kuwa wakati wastani wa kufaulu ni Alama 30, shule kwa Kanda ya Kusini-Lindi na Mtwara wanafunzi wake wameshindwa kabisa kufikisha wastani huo na wengi wao wameishia wastani wa 10 hadi 15! Ikumbukwe kuwa kuanzia mwaka 2012 wanafunzi watakaoshindwa kufikisha wastani wa alama 30 hatawaruhisiwa kuendelea kidato cha tatu bali watatakiwa kukariri kidato cha pili! Matokea ni mabaya sana, lakini swali la kujiuliza ni kuwa TATIZO LIKO WAPI?
Tatizo lipo kwa Sister Joyce!
Tatizo ni mgomo baridi wa walimu. Nipo ninafanya utafiti katika shule za sekondary na msingi jijini Dar es salaam. Nitawaleteeni hapa matokeo muone. Kusema ukweli ni kwamba walimu mashuleni hawana tena muda wa kufundisha. Wapo busy na biashara zao. Nitafungua thread na kuleta mchanganuo kamili wa nini kinaendelea mashuleni.
Mkuu Lukolo hapo bado sijaelewa, Mgomo huu ni wa kuigomea serikali au ni wa walimu kuwa bize na kazi Biashara zao, hata hivyo sio wote wenye Biashara!
Lakini si umeona waziri ametangaza matokeo ya kisiasa? Na yameonyesha ufauluu umepanda? Kazi ipo.Tumegoma:ndio maana mimi nilichukia sana mukoba alipotangaza mgomo.yaani alikuwa ana haribu dili.
Joyce ndiye anayefanya mitihani au ndiye anayewafundisha watoto? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Tuwe wakweli! au nawe uko kwenye ule msafara wa wale wanaodai misalaba ipunguzwe au iondolewe kabisa NECTA? :fencing:
Tatizo lengine ni kwamba kila mmoja naona mwenzake ndo anakosea, Viongozi wa elimu wanawaona walimu kuwa hawfanyi kazi vizuri, walimu wanaowaona wakuu wao wao wa shule wakorofi, wakuu wa shule wanawaona viongozi kuwa wamekosa sera na muelekeo na kuwa shule haziongozeki kwa kuwa hazina vifaa, walimu, vitabu n.k wanafunzi wanawalaumu walimu kuwahawafundishi na walimu wanaona wanfunzi wa kizazi hiki ni matatizo matupu, wazazi wanawaogopo watoto wao na wanaona walimu kuwa ni maadui wa watoto wao. basi imekuwa ni mvurugano mtupu!
Aluta kontinua.nchi hii mpaka wote tuokote makopo kwa uwenda wazimu.
Umenichekesha sana. Ni kweli Joyce kafanya kazi nzuri sana. Ila waabudu mwezi huwa hawaridhiki kwa lolote. Hupenda upendeleo tu.
sasa kaka mambo ya siasa na elimu yanaingiliana vipi?....wanafunzi wa siku hizii wameendekeza mapenz,usharobaro na usister duu tuuu na ndo maana wanafeli sana mitihanai yao....so cccm haihusiki apo kabisa ktk kufeli kwao mitihan.....