Matokeo ya Kidato cha Sita ni kanyaboya!

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Kuna taarifa za siri na kiintelijensia zinazobainisha kwamba matokeo ya Mitihani ya kuhitimu Kidato cha Sita (ACSEE) yamepikwa kisiasa. Inadaiwa kwamba matokeo hayo yalichakachuliwa (standardized) mara 3 na kikosikazi kilichopewa majukumu ya 'kuyaboresha' kabla ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kuyatangaza hadharani.

Habari zinabainisha kwamba baada ya matokeo ya kwanza kutoka, ambayo yalikuwa mabaya sana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr Shukuru Kawambwa, aliunda timu ya watu 6 ili 'kuboresha' matokeo hayo. Timu hiyo ilijumuisha watu wawili kutoka NECTA, watatu kutoka Wizara ya Elimu, na mtaalamu mwelekezi kutoka Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es laam, kampasi ya Mlimani.

Inaelezwa kwamba lengo kubwa la 'kuboresha' matokeo ni kuwavisha wazazi kilemba cha ukoka, hasa baada ya serikali kushindwa kuboresha kiwango cha elimu kwa vitendo. Ni matokeo yanayolenga kuwafurahisha wazazi na kuwafanya waamini kwamba kiwango cha elimu nchini kimepanda. Hii ni hatari kuliko maelezo!

:israel:
 
Kama data hizi ni sahihi kazi kweli kweli Unajua maana ya BIG RESULTS NOW?? Fuatilia matokeo haya ya kidato cha sita. Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne. Walitanua ukubwa wa goli ili iwe rahisi kufunga... Kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi zero 600 tu mwaka huu. Kutoka div.one 300 tu mwaka jana hadi one zaidi ya 4,000 mwaka huu.

Hivi waalimu walewale wa shule zilezile zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa
one 4,000 mwaka huu??

Changamoto zao zimetatuliwa? Maabara zimejengwa? Vitabu vimeongezwa? Madai ya walimu yamelipwa? Waalimu wa Kiswahili wameacha kufundisha Hesabu kutokana na ukosefu wa waalimu wa hesabu? Kama changamoto hizo zote hazijatatuliwa mabadiliko haya ya ghafla kutoka div.one 300 hadi div.one zaidi ya 4,000 yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kirahisi. Karibu Tanzania, hii ndiyo BRN bhana.!

Wanasema BRN means Big Results Now, mimi namwambia Waziri Kawambwa BRN, yani he should "Better Resign Now" maana watoto wetu wanapata BRN = Brain Receive Nothing.!!
 
CCM oyeeee, tumetekeleza ilani yetu ya uchaguzi kwa kufaulisha wanafunzi wengi. Ilani inahimiza ufaulu Tu, haiongelei suala la kama wana kitu kichwani au tulishusha marks. Huko University watajijua wenyewe kama watadisco shauri yao
 
100% ya hawa vijana wamefika umri wa kupiga kura 2015
 
Nothng to coment zaid ya kuugulia moyon inauma sana
 
Bado nawashangaa sana!!hivi mtu aliyefaulu vizuri kidato cha nne akifaulu vizuri zaid kidato cha sita kuna tatizo!!

ushirikishe ubongo wako japo kidogo.
 
watanzania bado tunadanganywa hadharan itatuchukua muda na hawa ndo wale matokeo yao hayakua mazuri kidato cha nne
 
100% ya hawa vijana wamefika umri wa kupiga kura 2015

serikali inacheza kamari na maisha ya watanzania kwa sababu za kisiasa. tatizo serikali ya CCM inajaribu kusiasisha kila kitu.
 
Bado nawashangaa sana!!hivi mtu aliyefaulu vizuri kidato cha nne akifaulu vizuri zaid kidato cha sita kuna tatizo!!

unaelewa unachosema au unahororoja tu?
 
watanzania bado tunadanganywa hadharan itatuchukua muda na hawa ndo wale matokeo yao hayakua mazuri kidato cha nne

hebu funguka zaidi mkuu.
 
Me naona tatzo litakuja kuonekana vyuoni, coz kama wanafunzi wamepigwa bust ya kupata one watakiona huko chuo. Mambo yata change completly na disco zitakua kama disco kwel yan kila weekend. Haha ha🙄🙄 yan had Me nna one wakat Me nlijua hapo ni Two. Eeeh
 

Nimeamini watanzania tuna ungonjwa wa kulalamika, yani matokeo yakiwa mazuri twalalamika eti viongozi wajiuzuru.

Yakiwa mabaya hivyohivyo pia, mnadai wamechakachua. Mnataka matokeo yaweje ili myakubali na kuyaamini. NECTA, imepewa dhamana kubwa ya kusimamia mchakato mzima wa mitihani nchini, hivyo inabidi tuheshimu kazi ya taasisi hiyo na siyo kulalamika tu.Sasa kama kila aina ya matokeo yanayotoka hamyaamini na mnadai yamechakachuliwa.

Je, mnataka nani asimamie Mchakato mzima wa mitihani ya taifa, ambaye mtamwamini?.Ndugu zangu tusitoea hoja tuu, kwa ushabiki wa kisiasa.
 
Haiwezekani watoto wafaulu hivi, ukawa safari hii baraza la mitihani lazima liwe na wawakilishi wa vyama vyote! Hi!hi!hi!
 
Acheni ujinga kuchochea maneno yenu, walimu wenyewe waliosahisha wanakili kuwa wanafunzi hasa wa Arts walifaulu sana, sasa nyie wehu wachache sijui mnachochea nini hapa.

Kwahiyo watu wafeli ndio mseme elimu ipanda..?
 

Kichaa hiki si bure.
 
Acha mfumo wa elimu wa nchi hii uendelee kutengeneza wajinga!!!!
 
Bado nawashangaa sana!!hivi mtu aliyefaulu vizuri kidato cha nne akifaulu vizuri zaid kidato cha sita kuna tatizo!!
Jawilat unaambiwa makocha wameongeza upana wa goli ili magoli yapatikane wewe bado hushangaii. Cc Elli
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…