Matokeo ya mtihani kidato IV Jumapili

Status
Not open for further replies.

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
1,233
Reaction score
406
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne nchini ya mwaka 2014, yanatarajiwa kutangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Jumapili wiki hii.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde (pichani), alitoa ahadi hiyo kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpwapwa mkoani Dodoma, kufuatia ajali ya moto iliyotokea Januari 20, mwaka huu na kuteketeza mali zote zilizokuwa kwenye bweni la wasichana 64 wa kidato cha tano na cha sita.

Dk. Msonde alikuwa miongoni mwa viongozi walioongozana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi-Elimu), Kassim Majaliwa, kwenye ziara ya kutoa pole katika shule hiyo.

"Zawadi niliyowaandalia ni taarifa kwamba Februari 15, mwaka huu, tutatangaza matokeo ya mitihani iliyofanywa na watahiniwa wa kidato cha nne nchini. Nasema ni zawadi kwa sababu sijaitoa mahali kokote, nyie ndiyo wa kwanza kuipata," alieleza Msonde.

Watahiniwa waliotarajiwa kufanya mtihani huo Novemba, mwaka jana ni 297,488 huku watanihiwa 245,030 wakiwa wa shule na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 52,448. Watahiniwa wa shule walioandikishwa ni wavulana 132,244 (asilimia 53.97) na wasichana 112,786 (asilimia 46.03).

Kwa kawaida, matokeo ya kidato cha nne hutolewa Aprili, lakini mwaka huu yatatoka mapema kutokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu. Walimu ni miongoni mwa watumishi wa serikali ambao hutumiwa kusimamia uchaguzi mkuu.

Kupitia ziara hiyo, Serikali imepeleka vitanda 64 ambapo magodoro 64 yalitolewa na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

Pamoja na misaada hiyo, aliahidi kupeleka madaftari, mikebe ya vifaa vya hisabati, kalamu na kumpa kila mwanafunzi aliyekuwa akiishi kwenye bweni lililoteketea fedha taslim ili anunue vifaa binafsi ambavyo havikupatikana kwenye misaada iliyotolewa na wasamaria wema.

Aliongeza kuwa shule hiyo itapelekewa vitabu vya aina zote kwa kiwango cha kila mwanafunzi kuwa na kitabu chake, vitakavyonunuliwa kutokana na Sh. bilioni 27 ambazo zimepatikana kutoka kwenye ‘chenji' ya ununuzi wa rada.

Pamoja na misaada ya mahitaji binafsi ya wanafunzi inayopelekwa na watu binafsi, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali, misaada mingine inayoendelea kupelekwa ni vifaa vitakavyowezesha kujengwa kwa bweni mbadala.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (LAPF), umepeleka mabati 92 yenye thamani ya Sh. milioni mbili.

Chanzo: Nipashe
 
Siku hizi yamepoteza ule mvuto kama ilivyokuwa miaka ya nyuma maana ufaulu umekuwa wa holela tu.
 
Shake Money,

Mkuu hii nembo ya NECTA Tanzania au maana hilo neno NATIONAL sio lenyewe unless unaongelea kitu kingne mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi yamepoteza ule mvuto kama ilivyokuwa miaka ya nyuma maana ufaulu umekuwa wa holela tu.
Sometimes huwa nawahurumia sana wadogo zangu! wanahitimu weengi kidato cha nne, halafu kinachowakuta ni uvundo tu..

Imagine wanamaliza 40,000+ halafu wanafeli 19,000+!

Unadhani hii labour force iliyofeli itapelekwa wapi?

Mwanzo wa kutengeneza panya road ndo huu huu.
 
Mkuu hii nembo ya NECTA Tanzania au maana hilo neno NATIONAL sio lenyewe unless unaongelea kitu kingne mkuu

I see!
hiyo error nimeiona mkuu. nimei edit haraka sana!

Btw, tujiandae na vifo vingine vipya vya watoto wetu ambao walitarajia mavuno makubwa sana wakati walipanda wakati wa kiangazi bila juhudi za umwagiliaji...
 
Siku hizi ni Kama darasa la Saba maana ufaulu utasikia umepanda asilimia 98 si mnajua mwaka wa uchaguzi
 
Nipende kuwatakia mandalizi mema ya kupokea matokeo yenu ambayo yatatolewa jumapili ya wiki hii kuweni na moyo wa furaha kwakuwa najua unajua nn ulikipanda ambacho ndicho utakacho vuna.
 
Hamnaga kufel cku hizi mkuu even form 4 leavers nowadays anasoma degree
 
NECTA Kutangaza Matokeo Ya Kido Cha Nne Tarehe 15/02/2015 Siku Ya Jumapili. Tutarajie Mavuno Mazuri Kwa Vijana Wetu.

Chanzo: Magazetini.
 
Walimu walioenda kusahiisha wangetupa lipot ya huko usahihishaji ulikuwaje.
 
Tunashukuru kwa taarifa kuwa matokeo yatatoka Jumapili. Lakini mie naona kuwaambia watu waliopata ajali ya moto kama zawadi yao ni kutangazwa kwa matokeo ni kama kuwakejeli.

Ikumbukwe kwamba waliomaliza kidato cha nne wanaosubiri matokeo sio sehemu ya waliopata ajali ya moto maana waliondoka shuluni mara baada ya kumaliza mitihani. Ajali ya moto inahitaji zawadi zenye lengo la kuwasaidia waathirika kufidia mali zao zilizoteketea, kinyume cha hapo ni kama kuwakejeli tu.

Viongozi wanapaswa kuwa makini na wanachokisema kwa kuzingatia mazingira halisi. Kueleza siku ya kutangaza matokeo ni jambo zuri ambalo limefanyika katika mazingira ambayo si muafaka

Well huo ni mtazamo wangu
 
Bora watangaze mapema, kuliko madogo kuwa na hofu.
 
bora watangaze mapema, kuliko madogo kuwa na hofu.
Ni kawaida ya matokeo mkuu. hata kama ungetangaziwa baada ya wiki 2, hofu iko pale pale, watakaojiua wako pale pale na serikali haitofanya chochote...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…