Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi huu yatachelewa

Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi huu yatachelewa

Mbute na chai

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
564
Reaction score
593
12th May 2013


email.png

Email



printer.png

Print






Philipo%20Mulugo.jpg

Naibu Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo


Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi huu yatachelewa ili kutoa nafasi kwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kurekebisha matokeo mabaya ya mitihani kidato cha nne ya mwaka jana yaliyofutwa na serikali mwezi huu.
Matokeo ya kidato cha sita ambayo huwa yanatangazwa mwanzoni mwa mwezi Mei mpaka sasa hayajatolewa na kwamba hayatatangazwa mpaka matokeo mapya ya kidato cha nne yatakaporekebishwa rasmi.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Philipo Mulugo alisema ingawa wakati huu ndio unaopaswa yatangazwe matokeo ya kidato cha sita haitafanyika hivyo hadi yatangazwe matokeo mapya ya kidato cha nne baada ya kufutwa.

Hata hivyo, akasema huenda yakatolewa pamoja au yakafuata wakati mwingine lakini mara baada ya kukamilisha kazi ya kurejea na kusahihisha matokeo ya kidato cha nne.

"Siyo kwamba yamechelewa kwani muda wa kujiunga na chuo ni Septemba hivyo haitawaathiri kwa hilo," alisema Mulugo.

Kuhusu hatma ya wanafunzi wa kidato cha nne ambao wapo mashuleni wanaendelea na masomo ya kidato cha sita, alisema kama kutakuwa na wanafunzi ambao wapo madarasani shule zilizowasajili zitakuwa hazijafuata mfumo wa elimu unavyoelekeza.

Alifafanua kuwa mfumo wa elimu kwa kidato cha nne ulibadilishwa na kwamba endapo mwanafunzi akifaulu anatakiwa kujiunga rasmi kidato cha sita Julai na si vinginevyo.

Alisema licha ya ucheleweshaji wa matokeo hali hiyo haikuwaathiri wanafunzi hao kwa kuwa ratiba ya kwenda masomoni haijaanza kwa mujibu wa kalenda ya shule ya serikali.

Serikali ilifuta matokeo ya kidato cha nne ya 2012 na kuiagiza Necta kuyaandaa upya kwa kutumia utaratibu wa usahihishaji na upangaji madaraja uliotumiwa mwaka 2011

Taarifa ilisema mfumo uliotumika mwaka jana na kusababisha wanafunzi kushindwa vibaya haukufanyiwa utafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika.

Matokeo hayo yaliyotangazwa mwezi Februari mwaka huu yalionyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi walishindwa mtihani.




SOURCE: NIPASHE

(Copied and pasted here from http://www.ippmedia.com/frontend/?l=54588 )
 
Wanawazingua vijana wanaongojea matokeo hayo, na kuathiri shughuli za taasisi nyingine kama bodi ya mikopo, n.k.
 
Sasa we mbona umeweka habar ya zamani sana hii????....leta kitu brand new
 
Back
Top Bottom