Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,986
- 5,058
Nina binamu yangu mtoto wa anko kamaliza form four 2012. Matokeo yake siyajui na sikuwa na mpango wa kuyafuatilia. Leo nilikuwa na shida na mjomba na simu yake ilikuwa haipatikani, katika kuulizia nikapewa namba ya huyo dogo ili kama yuko nyumbani aniunganishe na mjomba. Nilipompigia akapokea na kujibu, MIMI NI MAMA YAKE, X HAYUPO! akakata simu. Nikapatwa na mshangao kwani najua mke wa anko alifariki, nikapiga tena akanijibu vile vile. Sauti ni yake lakini. Nikamtumia msg kwamba nataka kuongea na anko mimi ni Y, akazima simu kabisa. Kama hali ni mbaya kwa nini usiombe msaada wa ushauri? Kwani ni wa kwanza yeye kufeli? Nawashauri wadogo unapokwama usikimbie matatizo kwa yapo na yataendelea kuwepo!