Matola tofautisha ndondo cup na ligi kuu, ibadilishe timu yako la sivyo hufai kuwa kocha wa mpira

amita bacha

Senior Member
Joined
Mar 10, 2017
Posts
180
Reaction score
411
Mechi ya leo kati ya Yanga na Lipuli tumeshuhudia mpira wa hovyo kutoka kwa timu ya lipuli zaidi ya dakika 40 wanajilaza makusudi kupoteza muda, mpira ni mchezo wa miguu unaoonekana sasa masuala ya kujilaza na kujiangusha unaondoa ladha ya mpira bora wakacheza basket huko.

Kwako kocha wa Lipuli, waelekeze na wabadilishe wachezaji wako ,aina ya mchezo mnaocheza unakera na kutia hasira yaani zaidi ya dakika 45 inapotea kwa ujinga ,yani contact kidogo unajua kitakachofuata ni kupoteza muda.

Na mpira ulivyoisha sikushangaa kuona mashabiki wa yanga kutaka kuwavamia lipuli sababu mtu kanunua tiketi, katumia nauli halafu anakutana na ujinga na ladha ya mpira mbovu.

Matola ibadilishe timu yako acheni umama, chezeni mpira hata twiga stars hawachezi hivyo.
 
Duuh dozi imewaingia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kubali tu bhana mmevutwa Sharubu. Shishi baby hakuwepo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N moja ya mbinu ya mchezo.....kama vp yebo nao wangelala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa mpira ule, soka bongo bado sana,bora uanzishwe mchezo wa kupoteza muda though huwez kumlaum mpinzan kutumia mbinu hyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga ndio wamesababisha lipuli fc walale uwanjani. Kwa sababu wameshindwa kuwafunga kama wangewafunga wasingelala. Inanikumbusha mechi kati ya mbao fc na simba ccm kirumba iliishia 1:3 Simba walishinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…