Matongoga Mwarabu toka Tunduru: Tiba ya kuongeza kumbukumbu.

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,315
Ni miti mifupi sana inayojulikana na watu wa Tunduru kwaajili tiba nyingi toka enzi na enzi za wakazi wa Tunduru Ruvuma. Ni ngumu kupata jina lake kisayansi au katika kiswahili fasaha lakini kwa wakazi wa Tunduru ni Matunda yanayopendwa sana.
Zifuatazo ni faida za matunda haya:
1. Huongeza kumbukumbu- Mung'unya kama pipi matunda 2 hadi 4 kwa siku au kulingana na uhitaji wako.
2. Uvimbe- Sugulia mahali palipovimba asubuhi na jioni.
3. Kuumwa na nyuki, nge au manyigu- Loweka kwenye maji kisha paka mahali ulupong'atwa.
4. Nguvu za kiume- Mung'unya kama pipi matunda 7 masaa mawili kabla ya tendo.
5. Nguvu za kike na ashki- Fanya kama namba 4.
6. Mbu- Ili using'atwe na mbu loweka matunda kwenye maji kisha paka mwilini kama mafuta ya mgando.
7. Harufu mbaya sehemu za siri- Lowesha matunda kiasi kisha kunywa glasi moja au mbili na unawe sehemu za siri.
8. Homa- Loweka matunda kiasi kisha weka kwenye beseni ingiza miguu.
9. Jino- Jino linalouma weka tunda moja kwenye jino linalouma bila kumung'unya hadi utamu wa tunda utakapoisha.
10. BP- Mung'unya angalau matunda 8 kwa wiki.
NB- Matunda haya husitawi hasa nyakati za mvua. Yanapatikana pia Songea.
 

Attachments

  • 1420894703843.jpg
    124.8 KB · Views: 410
  • 1420894911918.jpg
    146.8 KB · Views: 391
Tutayapataje sasa ss wa mwanza?

Kama una mtu unayemfahamu yuko kusini Tunduru Ruvuma mwambie akutumie matunda pori ya Matongo ga Mwarabu. Au nyakati hizi za mvua tembelea porini fananisha yanaweza kupatikana jacben90
 
Last edited by a moderator:
Angali tu usije kufananisha ukachukua la sumu
 
Jaman wadau dah mm nina mchumba nampenda kwel na anafanya kaz ktk kampun ya TIENS, lkn yy namuona anjar kbsa nifanyeje?
 
+Helydate acha ujinga malalamiko yako peleka kwenye jukwaa la mapenz na mausiano.tutolee ujinga wako umu. kwa wale wenye kuyataka matongo ga mwarabu mi nko pand za 2nduru utaniPM.
 
+Helydate acha ujinga malalamiko yako peleka kwenye jukwaa la mapenz na mausiano.tutolee ujinga wako umu. kwa wale wenye kuyataka matongo ga mwarabu mi nko pand za 2nduru utaniPM.

Huyo ndiyo kwanza post ya pili, msamehe bure ndiyo kwanza anajifundisha kutumia mtandao.
 
Kweli yapo huku ila kuna jina lake tunaliita nimelisahau,sikujua kama yana faida hizo.

hustawi sana wakati wa mvua.
 
Kweli yapo huku ila kuna jina lake tunaliita nimelisahau,sikujua kama yana faida hizo.

hustawi sana wakati wa mvua.

Ni kweli mkuu Deo Corleone. Yapo sehemu nyingi pia. Kuna siku nilikuwa na rafiki yangu daktari wa lishe toka chuo kimoja cha wasabato huko Canada. Alipoyaona akawa anakula hadi basi. Akanitajia kwa jina lake kisayansi ila nimesahau. Porini kuna hazina kubwa ya lishe na tiba ila weupe wametudanganya tusiamini kama mdau mmoja hapo juu. Ila wenye kuamini wanatumia na wanafaidika. Ndio maana Dr. MziziMkavu huwa a atupatia dawa wakati mwingine wanabeza watu ila wanaojua maana wanaleta shuhuda hapa.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…