Matonya amvaa Lady Jaydee, kisa picha ya udhalilishaji

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440


STAA aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa Bongo Fleva , Shabani Ramadhani ' Matonya ' ameibuka na kumvaa mwanadada Judith Wambura ' Jide au Lady Jaydee ' akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake .

Akizungumza na mwanahabari wetu, Matonya alisema anamtafuta Jide popote alipo ili amuulize kinaga ubaga kwa nini aliamua kuposti picha kwenye mitandao yake ya kijamii ikimuonesha akiwa hajitambui pasipo kumtaarifu.

"Nimeumizwa sana na Jide kwa kitendo chake cha kuamua kunidhalilisha kwa kiasi hicho tena akijua mimi ni mwanamuziki mwenzake na kama kuna kitu aliona simfurahishi kwenye mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi kuniita na kunikalisha chini na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye mitandao , " alisema Matonya .

Matonya alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza . Matonya akiwa mtungi .

"Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani , " alisema Matonya .

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.
 

Attachments

  • 1421470701862.jpg
    46.3 KB · Views: 19,291
SAsa kama ni picha ya kwenye video mpya anawasiwasi gani ? Acha tumdharau tutaprove badae tutakapoona video!
 
Kama ni picha ya kitu kilicho jikoni imevuja vipi? Siku hizi huu mtindo wa kuvujisha kazi umekuwa mkubwa halafu mnakuja kulalamika mitaani.
 
Utetezi wa Nini sasa?

Ngoja tusubirie hiyo video yake mpya😃😃😃
 
Sasa kelele za nini wakat umesha sema no video mpya khaaa hawa wasanii wetu bwana kaio kweli
 
Pumbavu kweli badala ya kuwavaa aliokuwanao LOKESHENI wakampiga na kuzisambaza anamtaka Jide!!!
 
Kama ni picha ya kitu kilicho jikoni imevuja vipi? Siku hizi huu mtindo wa kuvujisha kazi umekuwa mkubwa halafu mnakuja kulalamika mitaani.

Kuna mdau humu alisema huwa wanavujisha ili kupima upepo,waone response ya mashabiki ikoje?
 
Skendo kama hiyo kama ni mimi hata kama haikuwa video itabidi nitengeneze wimbo fasta na kurekodi video nimevaa nguo hizo hizo na kulala kwenye matope ili kumaliza skendo
 
Hakuna video, sema ndo kaamua kuitengenezea video, kuuwa hiyo issue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…