MATONYA; Nyota wa Bongo Fleva anayepaa kibiashara

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Posts
18,772
Reaction score
8,939
UKIANGALIA historia yake, hakika unaweza kusema amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kampeni za kuuaga umasikini.

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba, ameyapata mafanikio hayo kupitia muziki wa kizazi kipya ambao katika miaka ya hivi karibuni umekuwa na mvuto, na pia ni `biashara’ kubwa kwa wanaoweza kuzichanga vyema karata zao.

Tunamzungumzia Seif Shaaban, maarufu kama Matonya ambaye baada ya muongo mmoja wa kupigana kisanii, sasa anaanza kula matunda ya kipaji chake. Leo hii, Matonya wa kwenye muziki ni `milionea’ fulani hivi.

Na umilionea wake hakuurithi, bali ameusotea, akadunduliza na sasa ana jeuri ya kuitwa Mkurugenzi. Anamiliki biashara kadhaa, ikiwamo ya kuuza magari, lakini sasa amekuja na kitu kipya, hoteli yenye hadhi ambayo iko mbioni kuzinduliwa, baada ya kumtafuna msanii huyo zaidi ya Sh milioni 150.

Katika mazungumzo na gazeti hili hivi karibuni, Matonya amethibitisha kuwa ndiye mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo katikati ya Jiji la Tanga.

“Ni hoteli yangu, mali yangu iliyotokana na jasho la kazi yangu,” anasema mkali huyo ambaye aliwahi kuzushiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya na kukamatwa China, uzushi alioukana na kusema “sifanyi biashara hiyo, sifikirii kuifanya na wala sijawahi kukanyaga China”.

Anasisitiza kuwa, mafanikio yake yanatokana na kukuna kichwa na kutoa tungo na mashairi yenye hisia kali na mvuto kwa mashabiki wake, ndiyo maana ameweza kufanikiwa. “Tangu nianze muziki kazi zangu zimekuwa zikikubalika, nikaongeza idadi ya mashabiki wa ndani na nje ya nchi.

“Ndiyo maana kila kukicha nimekuwa nikipata mialiko ya kutumbuiza sehemu mbalimbali duniani, Ulaya, Marekani na hata Afrika nimezunguka,” anasema na kuhoji katika mazingira ya aina hiyo, kwa nini abaki katika maisha yale yale ya U-Matonya?

Anaongeza kusema: “Ndiyo maana mpaka hoteli yangu inafikia hatua hii, kila pesa imetoka mfukoni mwangu. Hata benki sijapiga hodi kukopa pesa ya biashara yangu hii ambayo natarajia kuizindua wakati wowote kuanzia sasa.”

Na wakati anajipanga kuizindua hoteli hiyo ambayo anaitafutia jina, Matonya yuko katika hatua za mwisho za kutoa kazi yake mpya kisanii, wimbo aliodai utakuwa gumzo unaoitwa Lesbian, yaani `Usagaji’. Katika wimbo huo, amewashirikisha wakali Abdul Naseeb `Diamond’ na Albert Mangweha `Ngwair’.

Kama ilivyo katika nyimbo zake zilizotangulia, nao umeangukia katika `mahaba’. Tofauti na mawazo ya wengi kuwa wasanii wanapaswa kubadilisha mwelekeo na kuachana na nyimbo za mapenzi, Matonya anasema nyimbo za mapenzi ndizo zinazouza.

“Kuna nyimbo nyingi za kusifia nchi, lakini hazifanyi vizuri sokoni ila nyimbo za mapenzi ndiyo zinauza,” anasema kijana huyo wa Kisambaa aliyekulia Barabara ya Tatu mjini Tanga. Miongoni mwa nyimbo za mapenzi zilizompatia umaarufu mkubwa Matonya ni pamoja na Anitha, Violeth, Taxi Bubu na nyingine kadha wa kadha.

Lakini kwa nini anaitwa Matonya? Mwenyewe anajibu: “Kweli kabisa nilikuwa napiga sana `mizinga’ marafiki zangu wakati nataka kurekodi kibao cha Uaminifu mwaka 2000, ndiyo maana wakaamua kunipa jina hilo nami nikalipokea.

Ndiyo, nilishajipanga kimuziki, lakini sikuwa na pesa za kuingia studio kurekodi, sikuona aibu kusaka pesa ya studio.” Anafafanua kuwa, wakati huo alikuwa kidato cha nne Sekondari ya Sahare iliyopo mjini Tanga.

Majibu yake yanatoa majibu mengine, ya kisa cha yeye kuitwa Matonya, jina la ombaomba maarufu nchini ambaye jina lake halisi ni Paulo Mawezi. Mzee huyo alipata umaarufu mkubwa baada ya `kusumbuana’ sana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba ambaye licha ya kumtimua mara kadhaa katika jiji hilo.

Staili yake ya kuomba kwa kawaida huwa ni `burudani’. Hulala chali huku mkono akiwa ameunyoosha juu kwa muda mrefu bila ya kutikisika hata kama jua ni kali kupita kiasi.

Huyo ndiye Matonya wa kwenye muziki ambaye baada ya kusota kwa miaka kadhaa, hatimaye ameanza kufungua milango ya mafanikio na sasa anatumia kila anachokipata kwa ajili ya ustawi wa maisha yake na familia yake na mkewe Miriam aliyezaa naye mtoto mmoja, Imran.

Je, atafanikiwa zaidi kibiashara? Bila shaka, kama ameweza kufika hapo, huenda akazidi kupaa na hivyo kutoa funzo kwa wasanii wengine nchini kuwa, kuna maisha mengine nje ya jukwaa la muziki.

My take:

Hivi huyu si nasikia si ameokolewa juzi juzi tu huko china kunyongwa?
 
Sasa mbona unaanza umbea tena? Inaelekea wewe ni mwandishi wa hilo gazeti! Sijui gazeti gani hata hivyo! Kuna swali juu ya biashara ya madawa ya kulevya na akajibu hausiki na hiyo biashara.
Haya mambo ya nasikia nasikia yanatoka wapi? China kuna kuokolewa kwa issue ya dope? Labda wamekudanganya waliokuambia!
 
'ngada' tu uyo,biz nyingine anazugia.
 
kwani,nini maana ya milionea?

acha dharau kwani m2 kuitwa bilionea anatakiwa awe na nini?af kwa kuangalia hatua alizopitia jamaa ndo kijana wa ktz inatakiwa afanye hvyo,hzo ishu nyingine za powder ni mapito!big up 2 him.
 
Yan kumilik kijihotel cha mil 150 ndo ajiite milionea?
Nampa hongera zake Ila hiyo Mil 150 yake ni faida ya biashara zangu kwa mwezi mmoja ,,Na hapo nimeshatoa gharama za uendeshaji,,
 
Baada ya kuchunwa kabaki na vichenji hivyo!Anyways,amejitahidi!
 
asee mi hata kibanda cha mbao cna,
kwangu mi ni milionea huyo,kuna yule mwenzie wa kuku kapanda
baisikeli anaishi tandale sababu hakuiheshim
ile pesa aliyokuwa anaipata,

big up sana tonya bwoi coz kuna wenzako wengi
hawawezi hata kupanga vyumba uswazi,
wanalala kwa mama dhao mpaka saivi navyoandika hii komenti!!!!!!!!!!!!!!!

kaza buti uwapatie watz vijana wenzio ajira


Yan kumilik kijihotel cha mil 150 ndo ajiite milionea?
 

I agree with you Flora, Penye haki lazima isemwe, tunadandia dala dala kila siku hata kibodaboda cha 900,000 hatuna, mwenzetu ana hotel ya thamani ya mil,150 .

Hastahili kuitwa Milionea....au kupata wapate wahindi tu akipata ngozi ya **** bado ni lofa?


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
hongera tonya boi japo watu wengi hawaamni na lazima kuna magumashi hapo kati hata kama ni powder ila hujakamatwa fresh tu maana hata hawa matajiri tunaojua wamepiga magumashi yakuzidi kufikia hapo. Ila hivi tzs 150m unatoa kitu cha hoteli?? Au gesti?? Sema tu ile kisanii tunaita hoteli....
 

tofali Tsh 100/=
mchanga na mawe bure!
Hotel ya miti hyo itakuwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…