BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Kuna muda huwa sipendi kupita katika njia ya pale Mwenge kwenye Jiji letu la Dar es Salaam hasa majira ya jioni, maana wale trafiki wanaoongoza magari mitaa hiyo ni wazinguaji hasa.
Kwa ufupi wao ndio wanaosababisha foleni iwe kubwa, bora wangeacha taa zifanye kazi, wanazingua sana.
Ikifika jioni, sijui huwa ndio wanataka waonekane wanafanya kazi au vipi, mfano nimefanya research isiyo rasmi ndani ya wiki mbili, kuna muda wanauweka upande mmoja kwenye break na kuruhusu upande mwingine kwa dakika 15
Hivi unapowasubirisha watu kwenye foleni kwa dakika 15 wakati upande wa pili wanapotakiwa kwenda hakuna foleni wala hakuna msongamano wowote, unategemea nini?
Sijui huwa wanapigiwa simu na watu wao kuwa upitishe upande huu ili wapiti fasta, nina hasira sana na trafiki wa kibongo, ukiachana na mambo ya ‘kutupiga’ sisi tunaoendesha vyombo vya moto, hili la pili nalo ni jibu
Naomba Serikali iangalie jinsi ya kufanya kuhusu usumbufu huu wa matrafiki kuwa sababu ya foleni