KERO Matrafiki wanadaiwa kuchukua pesa kwa makondakta wa daladala

KERO Matrafiki wanadaiwa kuchukua pesa kwa makondakta wa daladala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hii kitu inanikera sana na inaniacha na maswali mengi. Hii hasa ipo kwa magari ya Kawe pale karibu na kituo cha Jeshini, na njia ya kwenda Makumbusho kutokea Kinondoni Studio karibu na kituo cha daladala cha Vijana.

Askari hao wanasimamisha kila daladala inayopita na konda anakunja hela Tsh 2,000 kwenye kijikaratasi na kumpa askari aliyesimamisha gari.

Maswali ya kujiuliza
- Je, hile hela huwa ni ya nini?

- Na kwanini wanapewa kwa kuficha?

- Je huwa Serikali inaipata kwa namna gani?

- Je kwanini maaskari huwa hawakagui gari wanapewa pesa bila utaratibu?

inakera sana.
 
Back
Top Bottom