Matukio Halisi Yanayothibitisha Uchawi – Utashangaa!

Wanasemaga lisemwalo lipo na HILI la uchawi limesemwa kupitiliza,uchawi upo,ulikuwepo,na utazidi kuwepo.
Dunia ya leo tumekwisha toka kwenye issue za hearsay tunataka proof

Ukisema kuna
Mungu
Shetani
Malaika
Uchawi
Karma
na imani kama hizo inapwaswa ithibitishwe pasi na shaka vinginevyo ni HADITHI tu kama Hadithi za sungura na fisi
 
Acha utumbavu tafuta hela, sio mida wa hadithi huu... umeandika vizuri halafu umemalizia na tantalila... Gademningo
 
Dunia ya leo tumekwisha toka kwenye issue za hearsay tunataka proof

Ukisema kuna
Mungu
Shetani
Malaika
Uchawi
Karma
na imani kama hizo inapwaswa ithibitishwe pasi na shaka vinginevyo ni HADITHI tu kama Hadithi za sungura na fisi
Shida yenu hata akitokea mtu atakaetaka kuproove mnamuua,Vitu vipo ila MNATAKA mviongoze ninyi.Sitaongeza meseji nyingine zaidi ya hii.
 
Huenda wote waliofanikiwa wanaishi "kichawi ". Katika huu ulimwengu, upande wa giza ndio kila kitu. Taifa kubwa kama Marekani linatumia upande wa giza ila sisi wanatudanganya na dini.
 
Shida yenu hata akitokea mtu atakaetaka kuproove mnamuua,Vitu vipo ila MNATAKA mviongoze ninyi.Sitaongeza meseji nyingine zaidi ya hii.
Huwezi kuthibitisha ndio maana umejificha kwenye kichaka cha eti utauwawa ukithibitisha 😂

KITU KIPO na hauzi kuthibitisha uwepo wake
Hakuna mtu anayetaka kuongoza kitu hapa.... inatakiwa wewe ndio uongoze kuthibitisha
 
Huenda wote waliofanikiwa wanaishi "kichawi ". Katika huu ulimwengu, upande wa giza ndio kila kitu. Taifa kubwa kama Marekani linatumia upande wa giza ila sisi wanatudanganya na dini.
Masikini tuna matatizo sana
Yaani hapa kisaikolojia ni kwamba umehalalishi sisi kuwa masikini kwasababu haturogi kama wanavyoroga taifa kubwa USA 😂
 
Kiranga , Nyani Ngabu n.k tunawaita huku tunapenda kupata maoni na mitazamo yenu juu ya hii mada iliyo mbele yetu.
 
Huwezi kuthibitisha ndio maana umejificha kwenye kichaka cha eti utauwawa ukithibitisha 😂

KITU KIPO na hauzi kuthibitisha uwepo wake
Hakuna mtu anayetaka kuongoza kitu hapa.... inatakiwa wewe ndio uongoze kuthibitisha
Hata hapa jamii forums kuna kitu unaweza sema ukakuta usiku wa manane watu wapo pembeni ya kitanda chako.sio kila kitu kinasemwa na kuthibitishwa.Ndio maana hata Mungu haeleweki yupo au hayupo.
 
Zitakuja sahau miaka ya nyuma huko sumbawanga mwewe alimbeba ng'ombe mzima mzima anaruka maeneo angani akamla alafu mifupa ikawa inadondokea chini hii ishi ilitangazwa mpaka redioni
 
Unavyosema unaona kivuli
chake unamaanisha nini?
 
Kingine watu wanakuwa washirikina kupitia Imani za dini haya yanayoelezwa kuhusu kiongozi yule anayeumwa kuwa ni freemason si uongo ila sababu ni mambo ya Imani na tumezaliwa nazo hatuukubali ukweli huo ishara nyingi na matendo dhidi kuingia huko mfano kukubali mambo ya ushoga na hata kukataa maandiko ya vitabu vitukufu Kwa hoja ya upendo,baadhi ya wanaojiita manabii kuwa na nguvu wanazoziita miujiza lkn sababu ya binadamu na shida zao huukubali ushirikina huo na mtu huyo au baadhi ya viongozi wa dini kuvaa mapete makubwa yenye rangi za ajabu ambayo asili yake ushirikina upo kifupi asilimia kubwa tunafanya matendo ya kishirikina Kwa kutokujua au kujua ndio maana wenzetu kule misikini wanasema asilimia kubwa ya binadamu wataenda jehannam Kwa ushirikina nalikubali.
 
Ni kweli wanakuwa matajiri sana ila pesa zao zinatumika kununulia vitu vya kichawi tu
 
Dunia ya leo tumekwisha toka kwenye issue za hearsay tunataka proof

Ukisema kuna
Mungu
Shetani
Malaika
Uchawi
Karma
na imani kama hizo inapwaswa ithibitishwe pasi na shaka vinginevyo ni HADITHI tu kama Hadithi za sungura na fisi
Wewe nani aliyekwambia kuwa hayo mambo yanapaswa kuthibitishwa bila ya shaka? Mfano wewe hauamini hayo mambo na unaishi maisha yako kama kawaida sasa huo ulazima wa kutaka hayo mambo yathibitishwe bila ya shaka unatoka wapi?

Mimi siamini kuhusu Karma na naishi maisha yangu sioni haja kwa watu wenye kuamini Karma kulazimika kuthibitisha bila ya shaka kuhusu kuwepo kwa karma, sasa sijui wewe kipi kinakufanya uone wanapaswa kuthibitisha bila ya shaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…