Matukio Halisi Yanayothibitisha Uchawi – Utashangaa!

Ile part unasema alikuwa sebleni anasali afu we huku chumbani unaona kivuli chake naomba unieleweshe kidogo tafadhali
Hkuwepo chumbani but nikiwa nimelala alfajili yupo sebuleni nikiwa nusu macho namuona kama yeye anainuka kitandani kufumbua macho yote kapotea nipo peke yangu
 
Hkuwepo chumbani but nikiwa nimelala alfajili yupo sebuleni nikiwa nusu macho namuona kama yeye anainuka kitandani kufumbua macho yote kapotea nipo peke yangu
Nilipo amia kwenye nyumba mpya nilitaka kuikimbia nilikutana na Jambo Kama lako several times
 
Mwenye dawa ya kuwaua wachawi tuwasiliane wapumbavu sana hawa walala nje
Ilikua usiku wa mwanzo mwanzo nyumba mpya..hii nyumba ipo karibu na uwanja wa mpira wa miguu.

Nimelala usiku wa manane namwona mama mmoja bonge amekaa pembeni ya mke wangu Ile nafuta uso kuangalia vizuri akatoweka.

Siku ingine wife ananambia kambona paka mweusi anataka kunin'gata Ile anataka kumshika kapotelea mikononi

Ni BALAA SANAAA sisi tulichukua maji ya mwamposa na mafuta tukawa tunamwagia ndani pia kufanya maombi kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareth.

Pia Gly glue alikua MSAADA Sanaa alinishauri vyema Sana.
 
Kwahiyo wewe unataka mtu akiropoka tu kitu fulani kipo hata kama hakipo tukubali tu?
 
Uchawi haupo hizo ni propaganda na story za jaba
 
Kwahiyo wewe unataka mtu akiropoka tu kitu fulani kipo hata kama hakipo tukubali tu?
Kukubali ni hiari yako ndio maana nikasema kuwa mimi siamini kuhusu Karma lakini naishi maisha yangu hakuna anaenilazimisha nikubali kuwa karma ipo kweli, kwanza haiwezekani kuwa kila mtu akiropoka kitu basi wewe uanze kumdai uthibitisho utafanya hivyo kwa mambo mangapi?

Usitake kumzuia mtu anachoona yeye ni ukweli hata kama wewe unaona si kweli, ilimradi hakulazimishi kutu we ishi maisha yako mambo ya sijui kulazimika kuthibitisha hayana maana yeyote.
 
Mkuu unapo amini imani yako na ukabaki nayo hakuna atakaye kubughudhi....... uthibitisho unakuja unapo taka kuwaaminisha na wengine imani zako

Umesoma title na maelezo ya mleta mada lakini?
Mleta mada kaleta mada kwenye public forum ijadiliwe kwamba ana uthibitisho wa uchawi hadi tutashangaa👀
halafu wewe hutaki tujadili kwa kuhoji huo uthibitisho, hujioni kama wewe ndio mwenye matatizo zaidi?
 
Mkuu, hivi fisi og unamfahamu au unawajua fisi wa kwenye karatasi?

Fisi utamkamataje na kisha umgonge mhuri?

Simba mwenyewe kumkamata fisi mpaka apige mahesabu yaliyokamilika!

Binadamu aweze kutengeneza ndege inapaa juu halafu ashindwe kuwa na akili ya kumkamata fisi ?

Anamtega na chakula chenye nusu kaputi tu. Fisi analala mwenyewe anapigwa mihuri na kufanywa chochote
 
Msingi wa hoja yangu ni kwamba hakuna ulazima wenye kumuhitaji mtu mwenye kuamini jambo fulani kulazimika kuthibitisha, kwa maana hamlazimishi mtu mwengine akubali hicho anachokiamini yeye na inajulikana kuamini ni hiari tu hivyo hata mimi nikija hapa kutaka kukuaminisha nayoyaamini pia ni hiari ya watu wenyewe humu kuamua kukubaliana na ninachoamini au kutokubali basi na maisha yanaendelea ndio imani zilivyo.

Sasa kama mleta mada amedai ana uthibitisho basi ujadiliwe huo uthibitisho wake, ila hoja ya kwamba et imani yangu nikae nayo tu ila nikileta public basi nalazimika kuthibitisha hili ndio nalipinga.
 
Huu ni uzi mzito sana! Inaonekana umetumia mifano mingi inayotoka katika simulizi na imani za watu tofauti, hasa barani Afrika. Maswali kuhusu uchawi yamekuwepo kwa miaka mingi, na wengi wamejaribu kuyajibu kupitia dini, sayansi, na uzoefu wa maisha.

Swali kuu ni: Je, matukio haya yanaweza kuelezewa kwa njia nyingine tofauti na uchawi?

Kwa mfano:

1. Mtoto kunyoa nywele nusu usiku – Inaweza kuwa vitendo vya binadamu (labda mzazi au ndugu aliye na tatizo la usingizi) au hali fulani ya kiafya inayosababisha nywele kudondoka kwa ghafla.


2. Gari kuzimika kijijini – Hili linaweza kuelezewa kwa sababu za kawaida kama hali ya hewa, matatizo ya mfumo wa umeme, au hata mafuta machafu.


3. Utajiri wa ghafla – Mara nyingi watu hupata mali kupitia njia ambazo hazifahamiki kwa wengine, kama biashara za siri, urithi, au hata uhalifu.


4. Msukule na waliokufa kurudi – Inawezekana baadhi ya kesi ni za watu waliokosewa kuthibitishwa kifo chao, ama waliotekwa na baadaye kurudi.



Hata hivyo, kuna matukio mengine ambayo hayana maelezo rahisi, na ndiyo maana mjadala wa uchawi unaendelea.
 
IMANI bila kutumia akili ni ujinga kama ujinga mwingine wowote ule
Kwa mentality kama hizi no wonder the likes like Kibwetere na Mackenzie waliwateketeza waumini wao kwa kuwaaminisha ujinga ujinga

Mkuu unajua ni imani ngapi zimepigwa marufuku kwasababu ni za kipuuzi?
Just imagine kuna watu wanakata wenzao vichwa kwasababu wamehama uislam kisa imani yao
Wamasai walikua wana watupa porini watoto wanao zaliwa vilema kwasababu ya imani yao kuwa ni laana
Nyanza ya ziwa wazee wenye macho mekundu wamekatwa katwa sana mapanga na kuchomwa moto wakiaminika ni wachawi...... hii kwako imekaaje? Waachwe wamini wanavyotaka?

So ukimuelemisha mtu hakuna uchawi kwasababu hakuna uthibitisho hawezi tena kuwaua wazee wenye macho mekundu wala kutafuta viungo vya albino au kupiga ramli chonganishi

Ukimuelimisha mtu hakuna Mungu ataacha ujinga wa kuamini kukata wenzake vichwa au kukesha makanisani kuomba kutafuta favor kutoka kwa mungu asiyekuwepo
 
Unachotaka kufanya wewe ni kuondoa uhuru wa imani au kuamini ambao ni haki iliyo kisheria, imani potofu zinapingwa na watu wanaelimishwa hivyo usitake kuondoa uhuru wa imani kisa kuna baadhi ya imani ni potofu dawa ni kuelimisha watu sio kuwafanya kuwa atheists hiyo haitosaidia kutokuwa na imani potofu au kutotenda uhalifu.


Kila siku tunasikia matukio ya kinyama watu hufanya kwa sababu za kisiasa au unakuta kisa ni wivu tu wa mapenzi, watu wanaacha kufanya kazi na kukesha kubeti n.k hivyo mtu anaweza kufanya lolote kwa kutumia lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…