Matukio kumi ya kihalifu yaliyoitikisa dunia

Bitoz

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2015
Posts
30,823
Reaction score
126,553
Wakuu kama mnavyojua wahalifu ni sehemu ya jamii hata hapa jukwaani wamejaa tele
Sasa nataka kuelezea kwa ufupi tu matukio na wahalifu waliowahi kufanikisha wizi mkubwa kwa weledi uliotukuka pasipo kutumia nguvu kubwa

.......................................................................

10/French "Vacuum" Gang

Kuanzia mwaka 2006 huko Ufaransa liliibuka genge la Kihalifu lisilofahamika la vibaka wajanja wajanja ambao waliiba na kusafisha kabisa Supamarket kwa kutumia kifaa maalumu walichokibuni cha fagio la vakyumu
Waligundua udhaifiu katika utunzaji fedha wa Supermarket ya Monoprix na hivyo kutumia fursa vizuri kwa kubuni fagio hilo la kuiibia kwenye vacuum tubes za utumzaji fedha
Hadi kufika 2011 walikuwa washakomba USD 800,000 kwa kutekeleza matukio 15 yenye mafanikio mkubwa bila kushtukiwa
Kamera za CCTV zilambulia kuona watu waliovaa mask tu
Hawa jamaa walikuwa wakiiba usiku tu muda ambao "serikali huwa imelala"
 
9/2010 Credit Lyonnais Paris Burglars

Mwaka 2010 wezi waliotukuka walifanikiwa kuvunja na kuzana kijanja katika Benki ya Mikopo ya Lyon iliyopo katikati ya jiji la Paris na kuiba viboksi vya kutunzia vito na pesa vyenye thamani ya mamilioni ya Euro pamoja na pesa taslimu.
Walifaniliwa kuingia kupitia mbinu zenye weledi wa hali ya juu kijanja na kuvuruga mifumo yot ya ulinzi ma hivyo kuiba kiulaini bila kushtukiwa
Pia mwaka 2011 genge hilo lilifanya tukio lingine kama hilo la kufuru
Hadi sasa umekosekana ushahidi wa kiwezesha kuwashtaki
 
8/Carl Gugasian

Huyu ndiye Friday Night Bank Robber
Huyu ni kibaka maoni mwenye Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania huko nchini Marekani ambaye aliamua kuutumia usomi wake kufanikishia matukio ya kijambazi
Alipohitimu tu mafunzo ya kijeshi akaanza kuiba magari katika casino 8 tofauti na kuyatumia kwenye matukio yake ya kihalifu
Aliprmdelra zaidi kuiba kwenye mabemki siku za ijumaa ndiyo maana anaitwa Friday Night Bank Robber
Allifika dakika 5 kabla ya benki kufungwa na kutumia dk 3 tu kubeba mpunga na kusepa zake bila kukamatwa
Alikuwa akivaa rundo la nguo ili kuficha utambulisho wa umbo pia alivaa mask na kutembea kwa staili ya kaa
 
Huyo jamaa aliyeungua si jamaa wa muvi ya Fred & Jackson anahusika vp hapo..
 
7/Paris Modern Art Museum Burglary

Mwezi May mwaka 2010 mweizi alivunja Makumbusho ya Sanaa ya Paris na kuiba kazi za kisanii kama vile za Picasso and Matisse ambazo zilikuwa na thamani ya Euro milioni 100
Pablo Picasso na Henri Matisse

Wizi huo ukaja kugundulika keshowe asubuhi muda wa saa 1 na kuaminika kwamba vitu vilivyoibiwa vinawerza kufika thamani ya Euro Milioni 430
Hadi kufikia mwaka 2012 hakukuwa na mtu yoyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo
 
Huyo jamaa aliyeungua si jamaa wa muvi ya Fred & Jackson anahusika vp hapo..
Sijawahi kuitazama iyo muvi
Labda itakuwa ina uhusiano na jamaa
 
Tupe mbinu za kuingia magogoni tukamwibie jiwe funguo za hazina na marupurupu yote anayotunza pale ndani manake jamaa mkuda wa kubana fedha utadhani ni Mali ya babake
Umewaza mbali mkuu maana wezi wa bongoelimu ndogo wanaishia kuiba vimilioni kadhaa tu
 
6/Derek 'Bertie' Smalls
Huyu alikuwa ni mwizi aliyebobea huko Uingereza katika miaka ya 1960Kabla ya miaka ya 1970 alikuwa ni mwizi mwenye jina kubwa kwenye mitaa ya jiji la London
Mwezi Februari 1970 aliongoza genge lake liitwalo Wembley Mob kuvamia na kuiba pesa kiasi cha Pauni 240,000 (wakati huo ulikuwa ni mpunga mrefu kichizi) katika benki ya Barclays kiasi ambacho ni rekodi kwa kipindi hicho
Kisha akapanda treni na kutimkia jijini Paris kusikilizia upepo
Baada ya juahidiwa kupewa kinga na mwendesha mashtaka iwapo atakubali kuelezea wizi ulivyofanyika kwaajili ya faida ya Polisi siku zijazo alikubali kurudi na kutoboa siri ambapo genge zims lolipigwa mvua ya miaka 100 jela ila yeue akasamehewa

Huyu jamaa ni msaliti kwa wenzake hana tofauti na Yuda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…