Matukio takriban 7,000 ya ukatili dhidi ya wanawake yaripotiwa kufanyika nchini Kenya tangu mwezi Septemba 2023

Matukio takriban 7,000 ya ukatili dhidi ya wanawake yaripotiwa kufanyika nchini Kenya tangu mwezi Septemba 2023

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Ripoti ya usalama wa nchi ya kenya ya mwaka 2024 imeonesha kuwa kuna matukio zaidi ya 7,100 vya ukatili wa kijinsia yaliyorekodiwa tangu Septemba 2023.

Miongoni mwa matukio hayo, kesi 100 za mauaji ya wanawake zimeripotiwa tangu Agosti 2024.

Mmoja wa waathiriwa wa ukatili huu, Sarah Wambui, alisimulia masaibu yake baada ya kushambuliwa na mume wake aliyeishi nae miaka 20.

“Alinishambulia tarehe 18 Januari 2024,” alisema. “Alinichoma visu mara 38, hadi viungo vyangu vya ndani kama figo na ini vilijeruhiwa. Nimekuwa hospitalini hadi niliporuhusiwa kutoka mwezi Agosti.”

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita, Waziri wa mpito wa Mambo ya Nje na Waziri wa Mambo ya Ndani Musalia Mudavadi, alionesha wasiwasi alionao juu ya ongezeko la matukio ya ukatili dhidi ya wanawake nchini Kenya.

Soma pia: Mamia waandamana kupinga Mauaji ya Kikatili dhidi ya Wanawake

“Kaunti ya Nairobi imerekodi idadi kubwa zaidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia, huku Samburu na Mandera zikiripoti idadi ndogo zaidi,
” alisema Mudavadi.

“Kumekuwa na mauaji 100 ya wanawake kati ya Agosti na Novemba 2024. Uchunguzi wa matukio haya umekamilishwa na Idara ya Upelelezi wa Jinai, na kesi nyingi ziko mahakamani zikisubiri uamuzi.”


Maandamano ya kudai kukomeshwa kwa mauaji ya wanawake yalifanyika wiki mbili zilizopita, lakini polisi waliyasitisha maandamano hayo kwa kutumia gesi ya machozi na kuwakamata baadhi ya waandamanaji.

Kwa upande wake, Sarah Wambui amesema maisha yake yako hatarini kwani mwanaume wake, ambaye ametoka gerezani, ameendelea kumtishia. “Ameapa kunimaliza, na sasa niko mafichoni,” alisema mama huyo wa watoto wawili.

Wataalamu wa haki za binadamu wanasema mfumo dume na ukosefu wa ulinzi ni sababu kuu za mashambulizi haya. Njoki Gachanja, mtetezi wa haki za binadamu, alisema idadi ya visa vya ukatili inaweza kuwa kubwa kuliko inavyoripotiwa.

GBV.png

“Idadi kubwa ya matukio inatokea katika maeneo ya kipato cha chini ambako umasikini umechochea ukatili,” alisema Gachanja.

Takwimu kutoka Kituo cha Gender Violence Recovery Centre zinaonyesha kuwa mwanamke 1 kati ya 3 nchini Kenya amepatia ukatili wa kingono kabla ya kufikisha umri miaka 18, huku asilimia 38 ya wanawake walioolewa wakiripoti ukatili wa kimwili.

===========================================================


Kenya’s security report this year has been dominated by the violence and killings of women and girls, with more than 7,100 cases of gender-based violence since September 2023.

Included in that number are 100 documented cases of murder against women since August 2024.

Sarah Wambui said she was attacked one morning by her husband of 20 years.

“He attacked me on Jan. 18, 2024,” she said. “He stabbed me all over — 38 stabs from my face, the entire body, even my internal organs, my kidney and liver, were affected. I have been in hospital. I was discharged in August.”

Speaking last week, Foreign Affairs Minister and acting Interior Minister Musalia Mudavadi said the number of incidents of sexual and gender-based violence, or SGBV, against women worries security officers.


“Nairobi County recorded the highest number of SGBV cases, while Samburu and Mandera counties had the lowest incidents,” Mudavadi said. “There were 100 murders of women from August to November 2024. So far, the Directorate of Criminal Investigation has completed the investigations on these, and the majority are pending before court.”

Two weeks ago, hundreds of people took to the streets in Kenya, demanding an end to the killings of women. The protest was dispersed by police using tear gas and making arrests.

The response by police angered demonstrators, human rights groups, and women’s organizations. They accused authorities of not taking the attacks and killings of women seriously.

Wambui’s accused attacker is out of prison and has been threatening to kill her, she said. The mother of two has been moving from one place to another to avoid him.


“Right now, my life is in danger,” she said. “The perpetrator is out, and he has vowed he will finish me, and the case will be discarded. So I am actually in hiding.”

Human rights researchers say patriarchal views and a lack of protection are some of the reasons behind the attacks on women and girls.

Njoki Gachanja, a human rights defender, said the number of abused women may be higher than reported.

"Most of those numbers come from low-income areas where there is a lot of poverty and that is linked to a lot of violence. So, these numbers may sound staggering for people who are on the ground documenting these cases on a daily basis,” Gachanja said. “We know that there are more people who have not been covered by those who made the headlines, and this is a catastrophe that must be addressed by the government."

According to the Gender Violence Recovery Centre, one in three Kenyan women has experienced sexual violence before the age of 18, and 38% of married women have experienced physical violence.

The government has set up a security team to address attacks on women and ensure justice for the victims.

Source: VOA News
 
Back
Top Bottom