Matukio ya Kusikitisha Uwanjani

Kipigo cha mbwa mwizi walichopata YANGA kutoka kwa SIMBA SC pale taifa!
Wadau mtajazia ilikuwa lini vile?
Walikojolewa ngapi?
 
kiungo wa clabu ya Bolton Fabrice Muamba aliyeanguka uwanjani kwenye mechi ya FA dhidi y Tottinham hotspurs, na mechi iliahirishwa. Jamaa moyo wake ulisimama kwa dk78,...madaktari wanasema alikuwa amekufa kwa dk 78!
 

nilcheza mpira na Keny..........kwa tukio lile anadai hakumgusa kabisa Nadhir na alimruka wakatimchomba kauwahi mpira uliokuwa fifty fifty......hata yeye alishtuka tu Mchomba kawa kama kachinjwa!(samahani sana....na Mungu amuweke pema).
nitukio lililohusishwa sana na uchawi...nilikua sokoine siku ile na ilikua mara yangu ya kwanza na ya mwisho kugusa mpira tena kama mchezaji....hata wa mazoezi niliacha kabisa...nikabaki shabiki tu!
 
michael owen kuumia na kuvunjika mguu kulikopelekea kupotea kwenye mpira na kutolewa kwa machela ndani ya second ya 9 ya dk ya kwanza ujerumani 2002
 
Pia
kipa pesa mbili aliyeuliwa na daluga la mchezaji wa 44 KJ kule mbeya... miaka ya mwanzoni mwa 2000s
Pia kuna kipa wa AFC ya Arusha Nadhir Mchomba aligongana na mshambuliaji akafia hapo hapo uwanjani
 
ASee mkuu naikumbuka hii picha ya kwenye gazeti ilikua inaonyesha kama kachinjwa na panga shingoni
Kiukweli lilikua tikio la kutisha sana tushukuru Mungu kipindi hiko haya mambo ya mitandao ya kijamii hayakua yametamalaki kama leo hii
Mungu aendelee kumpumzisha golikipa Nadhir Mchomba mahala pema peponi
 
dhaira kufanikiwa kung'oa kaseja simba,


kipa Dhaira alikufa kwa kansa miaka michache iliyopita tena akiwa bado kijana akicheza ughaibuni
. hicho ndio cha kusikitisha na sio hicho ulichoandika wewe
 
Kuna mchezaji alikua anashiriki sijui mashindano ya uhai cup ya vijana anaitwa ngasa nafikiri alifariki pale taifa muda mfupi baada ya kufunga goli.. kijana huyo alikua akishangilia kwa kujirusha rusha kwa nguvu kwa kujibamiza kifuani wengi wanahisi kitendo kile kilistua moyo wake kilichopeleka umauti
 

Nakumbuka pia.. lilikua gazeti la dimba nadhani wakiweka hii picha.. siamini Kama lilikua nikiatu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…