Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinatolewa kuwa aidha maiti zimefukuliwa kwa mganga wa kienyeji na maiti hizo unakuta ni za watu ambao walipotea na kutafutwa na ndugu, au mtu kafia kwa mganga na mtu huyo alitoweka akawa anatafutwa.
Najaribu kuwaza ina maana hao waganga wameanza kuua watu siku hizi wakati wa sintofahamu hii au kuna ajenda ya watu wasiojulikana kutaka kujivua lawama na kuwasingizia waganga ili watu waache kupiga kelele kwa kuwa wataona ni matukio yanayofanywa na watu tulionao uraiani yaani waganga pale zinapotokea changamoto za kiufundi kwenye mambo yao au waganga kutoa kafara?
Napata mashaka huenda kuna kitu kinapikwa hasa ukizingatia kauli tata za wenye mamlaka kuonesha kuwa masuala haya ya utekaji ni "vijidrama" au wengine wakisema kujiteka tu kuteka ili watu wapate pesa, kauli hizi nilizichukilia kama kuufanya umma uone hakuna jambo la hatari na mambo yako shwari na waachane na kelele zinazodai kuna utekaji, kama waliweza kuita drama wanashindwa kuseti ajenda kuwa ni watu wanauawa kwa mganga?
Naona harufu ya mchezo mchafu katika hii ya maiti kufukuliwa kwa mganga, mganga kukiri kuua na kuwapeleka kuonesha miili, miili kukutwa ndani au nyuma ya nyumba ya mganga, mganga kuwazika watu porini au shambani, kuna harufu mbaya dhidi ya janga la watu wasiojulikana na hawa waganga. Yawezekana sasa kila anayepotea atakutwa kafa kwa mganga!
Pia soma:
- Polisi: Wafanyabiashara wawili waliodaiwa kupotea Songea, waliuawa na Mganga wa Kienyeji na kuzikwa
- Ndugu wa wafanyabiashara waliopotea waiangukia Polisi