LGE2024 Matukio Yaliyojiri kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa mkoa wa Mbeya

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mkoa iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watukatika Mkoa wa Mbeya ni 2,343,754; wanaume 1,123,823 na wanawake 1,219,926

Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa, hali iliyosababisha mji wa Mbeya kupewa jina la utani kama "The Scotland of Africa"

Majimbo ya Mkoa wa Mbeya ni pamoja na; Lupa, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe Magharibi, Busokelo, Kyela.

SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Halmashauri za Mkoa wa Mbeya

Busokelo, Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Rungwe.

Soma Pia:

Mbeya.jpg

MAMLAKA ZA MIJI
Jiji la Mbeya
Kata: 36
Mitaa: 181

MAMLAKA ZA WILAYA
Wilaya ya Busokelo
Kata: 13
Vijiji: 56
Vitongoji: 237

Wilaya ya Chunya
Kata: 20
Vijiji: 43
Vitongoji: 233

Wilaya ya Kyela
Kata: 33
Vijiji: 93
Vitongoji: 407

Wilaya ya Mbarali
Kata: 20
Vijiji: 102
Vitongoji: 712

Wilaya ya Mbeya
Kata: 28
Vijiji: 140
Vitongoji: 903

Wilaya ya Rungwe

Kata: 29
Vijiji: 99
Vitongoji: 459

Jumla Kuu
Kata: 179
Mitaa: 181
Vijiji: 533
Vitongoji: 2951

Hali ya Kisiasa

Katika mkoa wa Mbeya kumekuwa na ushindani mkubwa sana wa kisiasa ambao unatoka kwa CCM pamoja na CHADEMA licha CCM ameonekana kuendelea kuchukua nafasi nyingi zaidi kuanzia Serikali za Mitaa hadi majimbo.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 Halmashauri ya Mbeya yenye mitaa 179, CCM ilishinda 103, CHADEMA 74 na NCCR-Mageuzi mitaa miwili; Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya yenye vijiji 72, CCM ilipata 52, CHADEMA 20; Chunya yenye vijiji 69, CCM ilipata 66 na CHADEMA vitatu; Mbarali yenye vijiji 93, CCM ilipata 78 na CHADEMA 15; Kyela vijiji 92, CCM imepata 79 Chadema 13, wakati Ileje yenye vijiji 70, CCM imepata 53, Chadema 15 na TLP kijiji kimoja.Halmashauri ya Wilaya ya Momba yenye vijiji 86, CCM ilivuna 77 na CHADEMA 9 na Busokelo yenye vijiji 56, CCM ilipata 51 na CHADEMA 5.

Ukitazama pia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 katika majimbo ya uchaguzi 13 CCM walishinda viti 9 huku CHADEMA wakishinda viti 4 tu. Lakini kwa mwaka 2019 katika uchaguzi wa serikali za mitaa kulitokea dosari ambayo tulishuhudia CCM ikishinda viti vingi na wengine wakipita bila kupingwa katika uchaguzi huo.

Ukitazama pia katika uchaguzi mkuu 2020 nao pia katika jumla ya majimbo ya uchaguzi 7 CCM walishinda viti vyote. Sasa tunaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa tunatamani mamlaka husika kufanya kazi zao kwa uweldi bila kuonyesha kupendelea upande wowote ule, ili kila chama kishiriki vyema uchaguzi huu kwa uhuru na haki.

Pia Soma,
 
Leo huku patakuwa pamoto, patashika zitakuwa nyingi... naona nyuki wa mama akina Lucas Mwashambwa washasema wameridhika na mchakato :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:
 
Back
Top Bottom