Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania na pia ni makao makuu ya serikali, ambapo bunge na ofisi nyingi za kitaifa zipo.
Idadi ya Watu
Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Dodoma una jumla ya watu 3,085,625. Idadi hii inajumuisha wanaume na wanawake kwa uwiano ufuatao:
- Wanaume:1,512,760
- Wanawake: 1,572,865
- Bahi(322,526 ) Wanaume - 156,427 Wanawake-166,099
- Chamwino(486,176) Wanaume -236,583 Wanawake-249,593
- Chemba(339,333 ) Wanaume-170,837 Wanawake-168,496
- Jiji la Dodoma (765,179 ) Wanaume - 373,440 Wanawake -391,739
- Kondoa(244,854) Wanaume-124,379 Wanawake- 120,475
- Kondoa Mjini(80,443) Wanaume-40,153 Wanawake-40,290
- Kongwa(443,867 ) Wanaume- 214,475 Wanawake-229,392
- Mpwapwa(403,247) Wanaume- 196,466 Wanawake-206,781
SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mchanganuo wa Vijiji, Mitaa, Kata na Vitongoji kwa Mkoa wa Dodoma
1 Jiji la Dodoma: Lina Kata 41 Mitaa 222, hakuna vijiji Wala Vitongoji
2 Mji Mdogo wa Kondoa: Una kata 8 n Mitaa 36 hakuna vijiji wala Vitongoj
3. Wilaya ya Bahi: Una kata 22, Vijiji 59 Vitongoji 552 Hakuna mitaa
4. Wilaya ya Chamwino: Kuna kata 36 Vijiji 107 Vitongoji 813 Hakuna Mitaa
5. Wilaya ya Chemba: Kuna Kata 26 Vijiji 114 Vitongoji 488 Hakuna Mitaa
6. Wilaya ya Kongwa: Kuna kata 22 Vijiji 87 Vitongoji 385
7. Wilaya ya Kondoa: Kuna kata 21 Vijiji 84 Vitongoji 382
8. Wilaya ya Mpwapwa: Kuna Kata 33 Vijiji 113 Vitongoji 591
Mkoa wa Dodoma una jumla ya Kata 209 Mitaa 258 Vijiji 564 na Vitongoji 3211
Bonyeza Kiungo hiki kusoma majina ya Vijiji na kata
Hali ya Kisiasa Mkoani Dodoma kulingana na uchaguzi uliopita
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 Chama cha Mapinduzi (CCM) kilipata ushindi mkubwa ambapo wagombea wake walipita bila kupingwa katika maeneo mengi, hasa kutokana na vyama vya upinzani kujitoa katika mchakato huo wakilalamikia mazingira yasiyokuwa ya haki na wengine kuonekana fomu zao zilikuwa hazikidhi vigezo vya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi kutokana na kuonekana zina makosa kwenye ujazaji wa fomu hizo. Hii ilisababisha CCM kushinda karibu asilimia 100 ya nafasi za uongozi katika vijiji, vitongoji, na mitaa ya Dodoma
Vyama vya upinzani kama CHADEMA na ACT-Wazalendo vilijiondoa baada ya wagombea wake wengi kuenguliwa kwa madai ya sababu zisizoeleweka, huku serikali na CCM zikihalalisha mchakato huo. Hali hii ilileta mvutano na lawama kutoka kwa wadau n vyama vya upinzani na hivyo CCM kupat ushindi wa kishindo.
Pia soma:
- LGE2024 - TAMISEMI: Jumla ya vijiji 12, 333, mitaa 4,269 na vitongoji 64, 274 vitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
- TAMISEMI: Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2024 zitaanza tarehe 20 hadi 26, Novemba
- Wilaya ya Bahi watumia michezo ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Rais Samia kuzindua uandikishaji wa Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa Oktoba 11, 2024 - Dodoma
- LGE2024 - Rais Samia Kuzindua Rasmi Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa Oktoba 11, 2024
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Dodoma: Wapiga Kura wakiwa na Vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM Wakati wa Kujiandikisha
- LGE2024 - News Alert: - Dodoma: Rais Samia ashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- LGE2024 - Waziri Ndejembi ajiandikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Dodoma
- LGE2024 - Mbunge Martha Gwau Ahamasisha Wananchi Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
- LGE2024 - Msimamizi wa Uchaguzi Dodoma: CHADEMA wameweka mawakala 55 katika vituo 666
- LGE2024 - CHADEMA Dodoma mjini wadai kunasa majina feki ya wapiga kura
- LGE2024 - Wapiga Kura Dodoma ni kama wamegoma kujiandikisha, Waandikishaji wameamua kuwafuata nyumbani na kazini ili wajiandikishe
- LGE2024 - Mkuu wa Wilaya ya Chamwino awapa kazi maalum Wenyeviti CCM / Mabalozi kuhusu uandikishaji
- LGE2024 - Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ajiandikisha Dodoma
- LGE2024 - News Alert: - CCM yashinda 98.83% Wenyeviti Serikali za Mitaa