Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
HISTORIA
Kwa mujibu wa tovuti ya Mkoa wa Manyara, Mkoa huu ulianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 367 lililotolewa tarehe 27 Julai, 2002 na kuchapishwa katika gazeti la Serikali tarehe 2 Agosti, 2002 baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha ambao kabla na wakati wa kipindi cha Uhuru ulijulikana kama Jimbo la Kaskazini (Northern Province). Miongoni mwa Wilaya zilizounda Mkoa huo ni Mbulu na Maasailand ambazo sehemu kubwa iko katika Mkoa wa Manyara sasa. Wilaya hizo ziligawanywa kama ifuatavyo:- Wilaya ya Mbulu ilianzisha Wilaya ya Hanang mwaka 1969 na Hanang ikianzisha Babati mwaka 1985, wakati Wilaya ya Maasailand iligawanywa kwenye Wilaya ya Kiteto mwaka 1974 ambayo pia iligawanywa na kuanzisha Wilaya ya Simanjiro mwaka 1993. Baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha, Wilaya za Mbulu, Hanang’, Babati, Kiteto na Simanjiro ziliuunda Mkoa wa Manyara huku makao yake makuu yakiwa ni Babati mjini.
Mkoa wa Manyara unapakana na Mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki na Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro Upande wa kaskazini.
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Manyara ni watu 1,892,502; wanaume 954,879 na wanawake 937,623.
MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA MANYARA
Mkoa wa Manyara una mfumo wa kiutawala unaojumuisha mamlaka za miji na wilaya zinazoratibu maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mkoa huu unajumuisha mamlaka mbili za miji na wilaya tano, kila moja ikiwa na muundo wake wa kiutawala unaozingatia kata, mitaa, vijiji, na vitongoji.
Chanzo: TAMISEMI
1. Mji wa Babati una kata 8, mitaa 35, vijiji 13, na vitongoji 54.
2. Mji wa Mbulu una kata 17, mitaa 58, vijiji 34, na vitongoji 152.
Kwa ujumla, miji hiyo miwili ina jumla ya kata 25, mitaa 93, vijiji 47, na vitongoji 206.
Mamlaka za Wilaya
Kwa upande wa mamlaka za wilaya, mkoa wa Manyara unajumuisha wilaya tano;
1. Wilaya ya Babati ina mitaa 25, vijiji 102, na vitongoji 408.
2. Wilaya ya Kiteto ina mitaa 23, vijiji 63, na vitongoji 278.
3. Wilaya ya Hanang ikiwa na mitaa 33, vijiji 96, na vitongoji 416.
4. Wilaya ya Mbulu ina mitaa 18, vijiji 76, na vitongoji 361.
5. Wilaya ya Simanjiro ina mitaa 18, vijiji 56, na vitongoji 277.
Kwa ujumla, wilaya hizi tano zina kata 117, mitaa 393, vijiji 440, na vitongoji 1,946.
Mkoa wa Manyara una jumla ya kata 142, mitaa 93, vijiji 440, na vitongoji 1,946.
SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
MAJIMBO YA KIUCHAGUZI
Mkoa huu una Halmashauri (7) na majimbo saba (7) ya uchaguzi ambayo ni: Jimbo la Babati vijijini, Jimbo la Babati Mjini, Jimbo la Hanang, Jimbo la Mbulu vijijini, Jimbo la Mbulu Mjini, Jimbo la Simanjiro, na Jimbo la Kiteto.
HALI YA KISIASA
Katika mkoa wa Manyara Chama tawala CCM ndicho chama kinachoongoza kwa nafasi za uongozi katika ngazi ya serikali za mitaa kuwa chini yake kutokana na uchaguzi wa mwaka 2019 ambapo chama hicho kwa asilimia kubwa kilipita bila kupingwa baada ya vyama vya upinzani kujitoa katika uchaguzi mara baada ya kuona taratibu za kugombea nafasi hizo hazikuzingatia demokrasia.
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kwa matokeo ya jumla kwa nchi nzima Chama cha Mapinduzi kilishinda nafasi za uongozi kwa Vijiji 12,260 sawa na asilimia 99.9, Mitaa 4263 sawa na asilimia 100 vitongoji 63,970 sawa na Asilimia 99.4.
Aidha katika uchaguzi mkuu 2020 ulipeleka ushindi kwa Chama hicho na kupelekea wabunge wote wa majimbo ya mkoa huu kutoka Chama Cha Mapinduzi hivyo kudhihirisha ushindani mdogo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Na haya ni majimbo ya uchaguzi mkoa wa Manyara, Babati Mjini Pauline Philipo Gekul (CCM), Babati Vijijini : Daniel Baran Silo (CCM), Hanang’ :Mhandisi Samwel Hayuma Xaday (CCM), Kiteto : Edward Ole Lekaita Kisau (CCM), Mbulu Mjini : Paulo Zacharia Issay (CCM), Mbulu Vijijini : Flatei Gregory Massay (CCM), Simanjiro : Christopher Olonyokie Ole Sendeka (CCM).
Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 pamoja na uchaguzi mkuu 2025, inatazamiwa kuwepo kwa kuimarishwaji kwa demokrasia hasa katika kuleta uchaguzi huru na wenye haki ili kuchochea ushindani kwa vyama vyote vya siasa.
KUELEKEA NOVEMBA 27
- Rais Samia Kuzindua Rasmi Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa
- LIVE - Rais Samia anashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- LGE2024 - News Alert: - Waziri Mchengerwa afafanua kuhusu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, leo Oktoba 15, 2024
- Manyara: RC Sendiga apeleka nyama ya nyumbu kwa jamii ya Wahadzabe ili kushawishi kujiandikisha katika daftari la makazi
- LGE2024 - Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Mahakama yaipa Ruhusa TAMISEMI kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Mchengerwa: Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi, waweke pingamizi
- Polisi: Kuna chama cha Siasa kinapanga kufanya Vurugu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa
- Makalla: Chagueni wagombea wa CCM wale wa CHADEMA Mbowe kasema hawana ILANI ni hatari kuwa na kiongozi bila kuwa na Mkataba wa atakufanyia nini
- Askofu Konki: Mtanzania usiuze kura yako kwa wagombea
- Manyara: Wanawake Babati wataka kampeni za kistaarabu, uchaguzi ufanyike kwa amani
- Manyara: TAKUKURU yatangaza kufanya Uchunguzi kwa Wagombea 3 wa CHADEMA na mgombea 1 wa CCM kwa madai ya rushwa!
- Mbunge Gekul: Tuwalipe CCM kwa kura nyingi kesho
- Manyara: TAKUKURU yatangaza kufanya Uchunguzi kwa Wagombea 3 wa CHADEMA na mgombea 1 wa CCM kwa madai ya rushwa!
- Mchengerwa: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya saa 72
- ACT Wazalendo waelezea rafu walizokutana nazo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa