Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkoa wa Tabora una ukubwa wa takriban kilomita za mraba 76,151, na ni miongoni mwa mikoa mikubwa zaidi nchini Tanzania.
SOMA PIA
Idadi ya Watu
Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Tabora una jumla ya watu 3,391,679. Idadi hii inajumuisha wanaume na wanawake kwa uwiano ufuatao:
- Wanaume:1,661,171
- Wanawake: 1,730,508
- Tabora Manispaa(308,741)-Wanaume 150,416 - Wanawake 158,325
- Nzega Mji/ Mji wa Nzega (125,193) Wanaume 60,097 - Wanawake 65,096
- Igunga(546,204)- Wanaume 266,554 - Wanawake 279,650
- Sikonge(335,686)-Wanaume 165,309 - Wanawake 170,377
- Urambo(260,322)- Wanaume 127,424 - Wanawake 132,898
- Uyui(562,588)-Wanaume 276,261- Wanawake 286,327
- Kaliua(678,447) Wanawame 331,965- Wanawake 346,482
- Nzega vijijini(574,498) Wanaume 283,145 - Wanawake 291,353
- Mkoa wa Tabora una jumla ya vijiji 882 vilivyogawanyika katika wilaya 7(Tabora Manispaa hakuna vijiji).
-Mkoa wa Tabora una jumla ya vitongoji 3,744,
Hali ya kisiasa Mkoni Tabora
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 CCM ilishinda nafasi nyingi za uongozi ndani ya Mkoa wa Tabora katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019, CCM ilipata ushindi mkubwa, ambapo ilijinyakulia karibu asilimia 99 ya viti vya wenyeviti wa vijiji, vitongoji, na mitaa.
Katika maeneo mengi, wagombea wa CCM walipita bila kupingwa kutokana na vyama vya upinzani, kama CHADEMA, kujiondoa kwa sababu ya kile walichoeleza kuwa ni mazingira yasiyo ya haki kwenye mchakato wa uchaguzi na wengine kudaiwa hawakujaza vizuri fomu zao ivyo kujikuta fomu zao zikikataliwa.
Pia soma:
- TAMISEMI: Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2024 zitaanza tarehe 20 hadi 26, Novemba
- LGE2024 - TAMISEMI: Jumla ya vijiji 12, 333, mitaa 4,269 na vitongoji 64, 274 vitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
- LGE2024 - Tabora: Watu zaidi ya 150,000 watumia siku moja kujiandikisha daftari la kupiga kura uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024
- LGE2024 - Kauli za kuupoteza Upinzani Nchini zinavyopoteza Wananchi kujiandikisha kupiga kura Tabora
- LGE2024 - Tabora: Jamaa wanasa Madaftari ya Kupiga Kura Kituo cha Kujiandikisha yakiwa na Majina lakini hayana Saini