SoC02 Matumaini

SoC02 Matumaini

Stories of Change - 2022 Competition

Sisal

New Member
Joined
Aug 12, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Maisha kila siku yanatufundisha kitu ,kwa kila siku inapopita ndo kadri mafunzo tunapata lakin kwa wengine hupuuzia na kuona kama ni kitu cha kawaida na ndio makosa yanazid kujirudia kwa sababu hatujifunzi kutokana na kosa la mwanzo tulilolifanya lakini tukae tutambue kila pumzi na siku tuliyopewa ina dhamani sana huenda hutogundua leo lakini siku utakayo gundua itakuw ushachelewa lakini isikatie matumaini njiani bado uko na nafasi ya pili kukabiliana na udhaifu wako.

Na ndo kitu kilichomtokea msichana Miriam hakuwahi tambua kosa lake la kwanza akazidi rudia makosa bila ya kujitambua na ndo itafikia siku ya mwisho wa matokeo yake ya kutokubali makosa yake akapata ujauzito wakati yuko likizo ya kumaliza kidato cha 4 kuanzia hapo ndo akajua kumbe siku zote nilikuwa nafanya makosa

Basi matokeo yakatoka amefaulu kwa DIV 1 ya point 11 akachaguliwa kwenda mchepuo wa sayansi (PCB) kwa upande wake hakuwa na furaha kwa sababu alijua alichokifanya na bado aliendelea kufanya kosa kwa kutomshirikisha mtu na aliyempa akaikataa kila siku zilipozidi dalili zikazidi jitokeza akaamua fanya maamuzi magumu ya kutoa ili mradi tu asitoe uaminifu wazazi wake waliokuw nao

Kuanzia hapo maisha yake kwa sababu alitambua makosa yake alienda kumaliza elimu yake alihitimu kidato cha 6 na kuelekea chuo na kuhitimu vizuri kabisa kwa maana ya shahada zake mbili hakutaka kujiajiri isipokuwa aliamua kuwasaidia wasichana wanao fanya makosa na kutotaka kukubali makosa alichokitaka yeye ni kubadilisha kabisa fikra za watu anaona sababu ya yeye kupewa ten nafasi nyingine maana huenda angekufa lakini anaona dhumuni ya kuwa hai ni kuwafumbua makosa ya watu wanayofanya na kuwapa tena nuru na matumaini kwa kuwa kuna tena nafasi ya pili katika maisha.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom