Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Nyakati hizi ni vigumu jambo lolote kuendelea bila kuhuhusisha teknolojia, kila sehemu ni digitali (tehama) haijalishi huna maarifa ya kiteknolojia au lah!, mtu au jamii bila kwenda na teknolojia kwa sasa anakuwa amechagua kubakia nyuma. Ulimwengu wa sasa unamlazimisha mwanadamu kwenda na teknolojia ni tofauti sana na miongo kadhaa iliyopita nyuma.
Amewai kusema aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba kipindi cha uhai wake kuwa "Muogope sana Mungu na Teknolojia", katika tafsiri hisiyo rasmi ni kuwa teknolojia ina nguvu kubwa katika ulimwengu wa leo.
Utendaji wa majukumu mengi ya Serikali na sekta binafsi umeanza kujikita kwenye mifumo ya kidigitali ili kwendana na kasi ya Dunia, hasa kurahisisha mazingira ya utoaji na upokeaji huduma.
Tehama imewezesha huduma nyingi na muhimu kupatikana kwa uharaka na inaendelea kuleta matoleo chanya pale inapotumika kwa dhamira sahihi.
Licha ya Serikali kuanza kuwekeza zaidi kwenye mifumo ya teknolojia kwa lengo lilelile la kuwezesha huduma kwa wananchi kupatikana kwa haraka lakini bado hali ni tete kwenye ngazi za Serikali za Mitaa.
Ofisi nyingi za wenyeviti wa Vijiji na Serikali za Mitaa, Wenyeviti wa Vitongoji pamoja na watendaji wengi kwenye ngazi za Kata bado wanatumia mifumo ya kizamani ambayo ni kikwazo cha utendaji fanisi.
Mfano kuna nyaraka nyingi na muhimu uhifadhiwa katika karatasi na mazingira ambayo sio rafiki, wakati mwingine nyaraka hizi utegemewa mahakamani kama ushahidi kwenye kesi ambazo uamua hatima za watu.
Sio tu nyaraka hizo kuhifadhiwa kinyemera pia upo uwezekano wa kuzigushi kwa sababu mtu akiwa na nia ovu kuzipata ni rahisi. Ofisi nyingi za viongozi kwenye ngazi za mitaa na vijiji ni makazi ya viongozi hao, tujiulize katika Dunia ya sasa nyaraka hizi zinakuwa katika mazingira rafiki?
Katika hili hatuwezi kuwalaumu sana watendaji hao ambao wengi wao wanaitumikia jamii kwa utashi wao bila maslahi yoyote, mfano leo unaweza kupoteza nyaraka ambayo uliipata kutoka kwa Mwenyekiti ukimtafuta akupatie hata kopi ya nakala hiyo unaweza kukuta hana au anaanza kupekua makaratasi siku nzima, tukumbushane Dunia imeshatoka huku.
Leo hii ikitokea nyumba ya kiongozi wa ngazi za Mtaa au Kijiji imeungua moto au kupata mafuriko nyaraka za umma zinakuwa hatarini kupotea.
Sambamba hayo lakini pia viongozi hao hawana ujuzi wa matumizi ya teknolojia hasa mifumo ya kidigitali, basi kama wapo ni wachache sana, wengine hata hawana uelewa hata wa kuandika (typing) kwenye vifaa vya kidigitali kama vile kompyuta.Sina budi kusema hata hawana mafunzo ya kidigitali
Nini kifanyike Sasa?
Serikali lazima itambue kuwa uwajibikaji unatakiwa kwenda sambamba na mazingira rafiki ya kuhifandhi nyaraka za umma katika mifumo ya kidigitali.
Ni muhimu Serikali za Mitaa kuwezeshwa katika matumizi ya mifumo ya kidigitali kwa lengo mama la kuchochea utendaji katika ngazi hizo. Wawekewe mazingira mazuri ya kutumia vifaa vya kidigitali kwenye Ofisi zao, kama vile kompyuta.
Fursa kwa Wadau: Zipo taasisi Nchini ambazo utekeleza majukumu ya kutoa elimu za kidigitali lakini elimu hii kwa ukubwa imekuwa ikiwafikia watendaji walioko kwenye Serikali kuu hasa ambao wapo ngazi za juu.
Ni fursa ya wao kushirikiana na Serikali kuzifikia jamii za chini kwenye ngazi za Serikali za Mitaa na Vijiji kuzipa ujuzi katika matumizi tehama, hasa namna ya wanavyoweza kuoanisha maswala ya kidigitali na majukumu yao.
Viongozi hao kwenye ngazi hizo wakianza kunufaika na matumizi ya tehama itasaidia kuchochea uwajibikaji na kurahisisha huduma kwa waitaji.
Ujenzi wa mfumo jumuishi wa tehama: Serikali Haina budi kujenga mfumo unaozileta pamoja Serikali za Mitaa na vijiji kwa lengo la kuongeza WiGo wa kupata taarifa muhimu juu ya kinachoendelea kwenye jamii, mfano taarifa za kesi na matukio mbalimbali yanayoripotiwa yanaweza kuingizwa kwenye mfumo huo.
Hatua hii inaweza kupunguza mazingira ya kesi nyingi kuyeyuka na kuchochea uwajibikaji kwa viongozi kufanya uamuzi sahihi. Yapo madai kuwa zipo kesi nyingi za ndoa za utotoni, ubakaji, mimba kwa wanafunzi, ulawiti na matukio mengine uzimikia kwenye ngazi hizo.
Ikichunguzwa kwa umakini sababu ni kuwa taarifa za awali hazipo kwenye mfumo rasmi hivyo ni rahisi watuhumiwa kuwarubuni viongozi hao kwa kushirikiana na viongozi wengine kubadili nyaraka na maelezo kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Zipo taarifa nyingi muhimu zinafia kwenye ngazi za Serikali za Mitaa, ingewezekana uenda baadhi ya taarifa zingetiliwa maanani zingeweza kuchambuliwa na mamlaka husika kuthibiti baadhi ya vitendo vya uharifu.
Kama utakuwepo mfumo unaopokea taarifa kudhihifadhi, itachochea uwajibikaji na kuongeza umakini katika uamuzi na usimamizi, lakini pia itawesha Serikali kufahamu uhalisia wa kilichopo kwenye jamii na kuweza kuchukua hatua kwa uharaka endapo taarifa zilizoingizwa kwenye mfumo ni nyeti zinazoitaji ngazi za juu kuchukua hatua za haraka.
Serikali za Mitaa na vijiji ndio msingi wa Nchi utazamwe kwa jicho la tatu.

Upvote
3