Matumizi mabaya ya fedha kwa viongozi, yanavyo gharimu vilabu Tanzania

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Habari Wadau,

Pilika Pilika za Hapa na Pale Zimefanya Tupoteane Humu Ila Tupo Pamoja.

Nikiri Wazi Kuwa Nimeufuatilia Mpira Wa Afrika, Afrika Mashariki na Tanzania Kwa Muda Mrefu na Nikafuatilia Uendeshaji Wa Vilabu Tanzania, Nimegundua Kuwa Vilabu Vyote Vya Mpira Tanzania, Vina Matumizi Mabaya Sana Ya Pesa zao, Hali inayopelekea Umaskini Kwenye Timu husika na Kushindwa Kukidhi baadhi ya Mahitaji Muhimu Sana Katika Timu.

Matumizi Haya Mabaya Ya Fedha Yamekuwa Yakifanywa na Viongozi wa Club, na Kupelekea Wachezaji ambao ndio watu muhimu katika Club kukosa Stahiki zao za msingi, na Club kupata Ugumu katika Kujiendesha au kuongeza Gharama za Uendeshaji wa Club Ambao Hazina Mzingi.

Sababu Moja Kubwa Kuliko zote ni

1. SAFARI ZA VIONGOZI. Eneo Kubwa Ambalo Club za Tanzania Zinatumia Vibaya Sana Pesa Zake ni Eneo La Safari za Viongozi Ambalo Halina Umuhimu wowote wala Ulazima Wowote wa Viongozi Kusafiri. Hii tunaiona Kwenye Vilabu Vyote Vya Tanzania kam Simba, Yanga na Azam. Kumekuwa na Utaratibu wa Kuwa Kila Timu Inapokwenda Basi Hawa viongozi wa Club lazima Nao Waende, Lakini Swali la Msingi ni Je, Kuna Ulazima Wowote wa Hawa Viongozi wa Timu Kusafiri Na Timu?

Sote tunakubaliana kuwa, Viongozi wa Timu Kama Mwenyekiti wa Timu, Mwenyekiti wa Bodi na Wengine Sio Sehemu ya Benchi la Ufundi, na Hivyo Timu Inaposafiri kama kila Kitu kilipangwa sawa kuna kua hakuna haja ya Kusafiri na Timu kwasababu Hawana Msaada wowote Pale Timu inapo safiri zaidi Ya Kuwa “Mizigo” kwenye timu Kwa Kuongeza Gharama zisizo za Msingi.

Mfano Nimeona Simba Kwenye Nchi zote inazokwenda Inakwenda na Viongozi Wengi wa Timu na Taasisi Kama Simba, Ambao Hawa Umuhimu, wala Ulazima Wowote Wa Kwenda Na Timu. Nafikiri ni Baadhi Ya Ushamba Wa Viongozi kutokwenda Nchi Mbali mbali Hivyo Wanatumia Mgongo wa Timu kwenda na Timu kusafisha Macho, Kuchua Per day payment ambazo hazina ulazima Wowote.

Sina Shida kama Viongozi wa Timu na Taasisi kwa Ujumla kama wanasafiri kwa Kutumia Pesa Zao lakini Kama Wanatumia Pesa Za Timu huo Ni Utumiaji Mbaya Wa Pesa. Tamaduni hizi zimeenda hadi kwenye Vilabu vidogo kabisa na kuona Kuwa ni Haki na Nisawa kwa Viongozi wa Timu Kusafiri na Timu huku fika kabisa kuwa Hana Msaada Wowote.

Ni wakati sasa Wa Viongozi wa Club kuzionea Huruma Hizi Club na kupunguza Safari ambazo sio za Lazima kuokoa Pesa za Timu.
 
Huu ni mwandiko wa manara mtupu
 
Labda ziongelee club ndogo kama yanga, mtibwa, na kmc huko.. lkn timu kama simba wana bajet za kutosha.wameenda Niger na morroco na wachezaji wote isipokuwa wale majeruhi tu. ..wameenda na madaktri wapishi wahudumu mbalimbali na wengineo wengi na toka wameondoka itwachukua siku 18+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…