Matumizi mbalimbali ya Foil

Matumizi mbalimbali ya Foil

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Je, unayajua Matumizi mengi ya foili ya aluminium tofauti na kufungia au kufunika Vyakula?

Foili ina matumizi mbalimbali kama Ifuatavyo

1. Kunoa Mikasi

- Tumia foili kunoa mikasi iliyopoteza makali.

- Kunja foili mara mbili au tatu na ukate kwa kutumia Mkasi

- Tumia kukata mara kwa mara kwa kurudia kwa matokeo bora.

2. Husaidia kupunguza uvimbe machoni

- Weka vipande vidogo vya foili kwenye 'friza' kwa angalau saa 1.

- Weka vipande hivyo vya baridi juu ya macho yako kwa takriban dakika 20.

- Hii husaidia kupunguza kujaa kwa macho na uchovu

3. Kurejesha Mng'ao wa Vyombo vya Chuma

-Chemsha Maji na ongeza Kijiko cha amira

-Kisha weka foili katika maji hayo pamoja na vyombo vya aina ya chuma kama vile vijiko kisha loweka kwa dakika 10.

- Hii itasaidia vyombo vyako kuonekana vipya na kuwa na mng’ao tena

4. Kutunza Ubora wa nguo zinafuliwa kwa kutumia Mashine

- Tengeneza maduara ya foili kisha weka kwenye mashine ya kufulia pamoja na nguo

- Njia hii husaidia nguo zisiharibike haraka.

5. Kusafisha Vyoo

- Kunja foili kama maduara Matatu na uweke sehemu ya 'flushing' ya maji.

- Funika na uache kwa dakika tano, kisha tumia maji hayo kusafisha choo.

- Hii husaidia kung’arisha choo kwa kuondoa madoa ya Manjano.
 
duh! kuna ukweli hapa?
kama ndio, basi nilichelewa kujiunga jf, watu mna nondo za kutosha
 
Bila kuongelea matumizi yake kwenye shisha uzi bado haujakamilika kabisa
 
Back
Top Bottom