Matumizi saba ya baking Soda ( Magadi Soda)

Asante sana charminglady kwa somo zuri kama nini,natumai kuanzia sasa lazima nitalifanyia kazi.kweli nimeamini elimu haina mwisho.
 
Last edited by a moderator:
nilikuwa sijui kuwa magadi inaweza fanya vitu hivi asante cousin kwa kunifahamisha

ona hapa nimepaste:

2.Kuzibua sinki la jikoni.

Sinki la jikoni mara nyingi huziba na kugoma kupitisha maji machafu kwasababu ya mafuta na uchafu wa chakula.Mwaga kikombe kimoja cha baking soda kwenye tundu la sinki,kisha mwaga vikombe vitatu vya maji ya moto sana.Acha kwa angalao masaa manne kabla hujatumia sinki.Ni vyema ukafany ivyo usiku unapoenda kulala kwani sinki halitatumika adi asubuhi.



3.Kukata harufu ya mkojo chooni.


Kama unasafisha choo lakini bado kuna harufu mbaya ya mkojo.Chukua nusu kikombe cha baking soda changanya na nusu kikombe cha vinegar nyeupe kisha mwaga ndani ya choo na unyunyuze kwenye sakafu ,na baada ya nusu saa unaweza kudeki sakafu ili pabaki safi.
 
Mmmh! Kweli mjini shule, ahsante mamii kwa somo zuri
 
asante mamii, aisee naanza kesho...ngoja ni print hii kitu ili nisisahau
 
Asante kwa somo,ila mi nataka kujua upatikanaji wa bicarbonate of soda,kama kuna ambazo wanapark nyingi kama 1kg au zaidi?maana madukani nakuta vile vipakti vidogo vidogo
 
Kumbe haifai kwa kula kama inafanya kazi zote hizo za usafi
 

Asanteee
 
baking powder sio bicarbonate of soda, rekebisha hapo kwanza. Which is which?
 

Good infor to share
 
Asante chaminglady~hii ni shule tosha lakini wasiwasi wangu ni kuwa matumizi haya makubwa ya hii baking soda hasa kwenye mapishi ya mikate,mandazi,mboga mbalimbali si kutakuja kuwa na athali kubwa za kiafya baadae,ni wasiwadi tu!i remain to be corrected😕
 
Ile harufu chukizi kwa firji ishapata dawa!wife,fuata maelekezo ya Charminglady!raha ya mfumo dume hii!natoa maelekezo tu!(joking)mimi nateswa na mfumo jike kiukweli ila naona fahari kuutumikia!
 
Shukrani mum... Umeona matumizi ya baking powder yameongezeka eeh??? Si.kwa ajili ya kuokea tu!!

Mama, kikombe cha ukubwa gani...cha chai, maji ya kunywa au kile kidogo cha kahawa chafu za mjini? au kama kombe la kunywea mbege?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…