Matumizi sahihi ya dawa

Matumizi sahihi ya dawa

osc michael

Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
55
Reaction score
95
MATUMIZI SAHIHI ya dawa yanamaanisha kuwa dawa sahihi imetolewa kwa mgojwa sahihi na kwamba imetumika kwa njia sahihi, kwa dozi sahihi, kwa wakati sahihi, kwa muda sahihi na kwamba gharama ni sahihi kwa mgonjwa husika na jamii yake kwa ujumla.


DAWA SAHIHI
Inahitaji kujua mgonjwa kwa u usahihi na dawa ambayo inafaa kutumika. Kwa mfano, kama tatizo limesababishwa na bacteria ni vema kutibu ugonjwa kwa dawa yanamaanisha kuua bacteria. Kazi hii hufanywa na daktari hivyo ni vema kila anapokuwa na ugonjwa umwone daktari.

MGONJWA SAHIHI
Zipo dawa zinatumika kwa watu wazima tu na nyingine kwa watoto tu, Kuna dawa ambazo haziruhisiwi kutumika kwa wajawazito na wanaonyonyesha, pia Zipo dawa zinaweza kuingiliana na dawa zingine ambazo mgonjwa anatumia. Hivyo ni vema kutoa taarifa za kutosha ili dawa sahihi itolewe kwa mgonjwa sahihi.

NJIA SAHIHI
Zipo dawa zinatolewa kwa njia ya kumeza, sindano, kupaka, na nyinginezo. Ni vema ukawasiliana na mtaalamu was afya ili afahamu ugonjwa wake kwa undani na kushauri njia sahihi ya kutumia dawa. Mfano, matumizi ya dawa kwa njia ya sindano pasipo na ulazima hayakubaliki.

DOZI SAHIHI
Dozi ni kiasi cha dawa ambacho mgonjwa anatakiwa kutumia kwa wakati mmoja. Kama unaumwa na ukaambiwa umeze vidonge viwili kila baada ya masaa nane, vidonge viwili ndio dozi yenyewe. Mgojwa asipotumia dozi sahihi hata hatapona vizuri. Mgojwa akimeza kiasi kikubwa zaidi ya dozi sahihi anaweza kuzidiwa nguvu na dawa, kudhoofika au hata kufariki. Hivyo, meza dozi sahihi kama ulivyoelekezwa na wataalamu was afya

WAKATI SAHIHI
Ukiambiwa meza mara moja kwa siku ni vema kuchagua Saa ya kumeza na kuendelea kumeza saa hivyo kila siku mfano kila siku saa moja asubuhi. Kama umeandikiwa kutwa mara mbili image maana umeze kila baada ya masaa 12, na kutwa mara tatu inamaana umeze kila baada ya masaa 8 na kwa muda huo huo kila siku.

MUDA SAHIHI
Ili kuweza kupona vizuri na kuzuia usugu wa magonjwa ni lazima kumeza kwa muda wote ulioelekezwa na mtaalamu wa dawa. Kuna dawa za kutumia kwa dozi 1 tu, kwa siku 1, 2, 3, 4, 5, 6, wiki 1 au zaidi, mwezi 1 au zaidi na wakati mwingine hutakiwa kumeza dawa kwa maisha yoke. Aidha unashauriwa unapopata tatizo lolote kutokana na utumishi wa dawa usikatishe dawa kiholela. Muone mtaalamu was huduma za afya.


GHARAMA SAHIHI
Gharama za dawa na matibabu inabidi ziwe sahihi na nafuu ili wagonjwa waweze kuzimudu na kukamilisha matibabu yote. Kuna wakati mwingine Madaktari au wauza dawa wanawapatia wagonjwa dawa za gharama kubwa ili hali Zipo za bei nafuu ambazo zinaweza kutibu ugonjwa husika (tabia hii inajitokeza hasa kwenye sekta binafsi)

JE HALI YA UTUMIAJI DAWA SAHIHI IKOJE ?
Kulingana na takwimu za shirika la afya Duniani, zaidi ya 50% ya dawa zinaandikwa, zinatolewa au kuuzwa bila kufuata utaratibu. Aidha, zaidi ya nusura ya wagonjwa hawatumii dawa kama inavyopasa.

Utafiti uliofanywa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto mwaka 2014 unaonyesha kuwa matumizi ya yasiyo sahihi ya dawa yanazidi kuongezeka hapa nchini. Kwa mfano matumizi ya dawa aina ya ya antibiotic na uchomaji was sindano usio kuwa walazima umeongezeka mara dufu.

Pia, tafiti mbalimbali zinaonyesha
  • tabia za wagonjwa kutokamilisha muda wa kumeza dawa hasa pale nawaposikia wamepata nafuu
  • baadhi ya wagonjwa hununua dawa katika maduka ya dawa bila kuandikiwa na daktari
  • baadhi ya wagonjwa hutumia vyeti vya wagonjwa wengine na kununua dawa bila ushauri wa daktari .
  • Baadhi ya Madaktari huandika na kutoa dawa nyingi kwa wakati mmoja bila umuhimu kwa mgonjwa (polypharmacy)

MADHARA YA KUTUMIA DAWA VIBAYA NI YAPI ?
  • kushindwa kupona magonjwa vizuri na kujirudia rudia kwa magonjwa
  • kuongezeka kwa usugu wa dawa aina ya antibiotic
  • kusababisha vifo na vilema
  • kuharibika kwa mimba na watoto kuzaliwa na ulemavu.
  • kuongezeka kwa gharama za matibabu kunakosababishwa na kupungua kwa ufanisi wa dawa.
 
Back
Top Bottom