Kuna watu wengi ambao bado hutumia baadhi ya maneno ya kiswahili kimakosa. Leo nimeona kidogo nielekeze japo kwa ufupi usahihi wa matumizi ya baadhi ya maneno
1. Tafadhali sema, Huu ufunguo na siyo hii funguo
2. Huu wimbo na siyo hii nyimbo, ila hizi nyimbo (katika wingi).
3. Usiseme amesharudi kazini, kumaanisha kutoka kazini, sema, umeshatoka kazini au umesharudi kutoka kazini
4. Usiseme, alikuja siku ya Jumapili, sema alikuja Jumapili, kwa sababu inajulikana Jumapili ni siku.
5. Usiseme shati jingine, sema shati lingine.
Naomba kuwasilisha.
BelindaJacob,No 3. Je unaweza kusema nimerejea kutoka kazini ikamaanisha sawa na nimesharudi kutoka kazini? Au hiyo kurejea inatumikaje hasa?
Mara kadhaa pia najiuliza kama ni sawa kusema nimeenda nyumbani kwa mtu na kumkuta hayupo,kama siyo je usahihi wake hapa ni nimeenda nyumbani kwa mtu na kukuta hayupo au laa?? Inanichanganya
Ukishasema 'nikakuta', tunatarajia kuna kitu ulichokikuta. Kama ndivyo basi ni vema ukakitaja ulichokikuta. Vinginevyo ni afadhali kusema: Nilienda nyumbani kwake hakuwapo (hakuwepo?). Hapo tutaelewa kwamba hukumkuta.BelindaJacob,
Unapokosea ndipo wengi wanapokosea.
Naweza kusaidia mwishoni tu, ya mwanzo ngumu kwangu.
Unatakiwa kusema:
Nilienda nyumbani kwake nikakuta hayupo.
au
Nilienda nyumbani kwake sikumkuta.
Sentensi mbili hapo juu ndizo sahihi
BelindaJacob,
Unapokosea ndipo wengi wanapokosea.
Naweza kusaidia mwishoni tu, ya mwanzo ngumu kwangu.
Unatakiwa kusema:
Nilienda nyumbani kwake nikakuta hayupo.
au
Nilienda nyumbani kwake sikumkuta.
Sentensi mbili hapo juu ndizo sahihi