Matumizi sahihi ya Maneno ya Kiswahili:

Matumizi sahihi ya Maneno ya Kiswahili:

Mwawado

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2006
Posts
993
Reaction score
259
Je unakubaliana na huyu Muungwana anayeandika matumizi ya haya maneno hapo chini?

Si vibaya tukapeana japo nyepesi nyepesi za lugha ya kiswahili baada ya kuonekana watu wengi kuitumia lugha hii ndivyo sivyo. Kwa uchache labda nichambue matumizi ya maneno yafuatayo.

1. Kuonyesha hali ya utashi baina ya vitu viwili. Wengi wetu hutumia, ...naweza panda aidha daladala au nikatembea. Usahihi wa hapa ni kwamba naweza panda ama daladala au nikatembea.

2. Tendo la kupiga mpira ili uweze kumkuta mchezaji mwingine. Wengi husema,...Juma alimpasia Hamad kabla ya kufunga bao. Usahihi ni kwamba, Juma alimpa mgongeo Hamad kabla ya...

3. Tendo la kutafasiri maana toka lugha moja hadi nyingine moja kwa moja. Wengi husema,...jamaa katafasiri moja kwa moja. Usahihi ni kwamba, ...fulani kafanya tafasiri sisisi.

4. Tendo la kupenyeza kitu kwenye tundu au kijishimo, mfano matumizi ya kadi ya ATM wakati wa kuchukua pesa. Wengi wetu husema ama kuingiza au kuweza. Kiswahili fasaha ni kubokoza kadi...

5. Binti mrembo apatikanae baada ya mashindano fulani ya urembo huitwa misi. Usahihi ni ama mlimbwende au banati. Mfano, ...juzi tulikwenda kushuhudia mashindano ya mabanati wa Tabata.

6. Mauaji yatokanayo na vita huitwa mauaji ya halaiki wakati usahihi ni mauaji ya kimbari...

7. Makubaliano ambayo yatamaliza uhasama wa muda fulani ambayo kwayo pande kinzani zitaweka ushuhuda wa maandishi, hii ilizoeleka kama azimio...usahihi wake ni mwafaka. (Azimio hutumika pale mtu au kundi fulani wanapotoa tamko na mara nyingi likionyesha muda ufuatao)

8. Hali ya kutokuwa na fedha hutumika kama ukwasi...usahihi wake ni ukata. (ukwasi huonesha utoshelevu na pengine ziada ya fedha)

9. Hali ya kuwa unadaiwa kiasi fulani cha fedha ili kutimiza hadi yako fulani watu huita balansi au salio. Usahihi ni bakaa.

10. Jini mkubwa ambaye husadikika kuishi kwenye miti mikubwa kama mbuyu huitwa subiani na wala si. pepo (Kinyamkela huwa ndiye pepo ambaye hupungwa/kufukuzwa kwa ngoma inayokesha)
 
Ajianzie yeye mwenyewe kwanza.

baada ya kuonekana watu wengi kuitumia lugha hii ndivyo sivyo

Watu wengi kuitumia? sio watu wengi wanaitumia? Ndivyo sivyo, how colloquial can he get?

Kwa uchache labda nichambue matumizi ya maneno yafuatayo.

Kwa uchache wa nini? Kwa haraka labda, kwa uchache?

1. Kuonyesha hali ya utashi baina ya vitu viwili. Wengi wetu hutumia, ...naweza panda aidha daladala au nikatembea. Usahihi wa hapa ni kwamba naweza panda ama daladala au nikatembea.

Right, watu wanachanganya neno la kiingereza "either" na neno la kiswahili "aidha". Neno "aidha" halitokani na "either" na wala halina maana sawa.Wakati "either" katika kiingereza linaashiria uchaguzi wa vitu viwili likitumika na "or", katika kiswahili "aidha" maana yake ni "pia" = "also" katika kiingereza.

2. Tendo la kupiga mpira ili uweze kumkuta mchezaji mwingine. Wengi husema,...Juma alimpasia Hamad kabla ya kufunga bao. Usahihi ni kwamba, Juma alimpa mgongeo Hamad kabla ya...

Mwambieni aangalie maana ya neno "kutohoa" katika kamusi ya kiswahili, na atafute neno hili la kupasi humo humo.

3. Tendo la kutafasiri maana toka lugha moja hadi nyingine moja kwa moja. Wengi husema,...jamaa katafasiri moja kwa moja. Usahihi ni kwamba, ...fulani kafanya tafasiri sisisi.

Anaonekana hakosoi ila anatoa maneno mbadala ya kiswahili.Huyu angekuwa muingereza angetaka Kiingereza kisiwe na maneno yenye asili ya Kilatini, can you imagine that?

4. Tendo la kupenyeza kitu kwenye tundu au kijishimo, mfano matumizi ya kadi ya ATM wakati wa kuchukua pesa. Wengi wetu husema ama kuingiza au kuweza. Kiswahili fasaha ni kubokoza kadi...

Mwishowe ataleta matusi sasa, mpaka kubokoa!

5. Binti mrembo apatikanae baada ya mashindano fulani ya urembo huitwa misi. Usahihi ni ama mlimbwende au banati. Mfano, ...juzi tulikwenda kushuhudia mashindano ya mabanati wa Tabata.

Hata kijana wa kiume anaweza kuwa mlimbwende, ulimbwende ni utanashati uendao na mitindo na usafi, definition yake narrow.

6. Mauaji yatokanayo na vita huitwa mauaji ya halaiki wakati usahihi ni mauaji ya kimbari...

Si kweli, mauaji ya kimbari ni ethnic cleansing, mauaji ya halaiki ni genocide, na si lazima mauaji yatokanayo na vita yawe any of the two. Again, shallow definitions.

7. Makubaliano ambayo yatamaliza uhasama wa muda fulani ambayo kwayo pande kinzani zitaweka ushuhuda wa maandishi, hii ilizoeleka kama azimio...usahihi wake ni mwafaka. (Azimio hutumika pale mtu au kundi fulani wanapotoa tamko na mara nyingi likionyesha muda ufuatao)

Hakuna sababu muafaka usiazimiwe. This thought process is not well thought.

8. Hali ya kutokuwa na fedha hutumika kama ukwasi...usahihi wake ni ukata. (ukwasi huonesha utoshelevu na pengine ziada ya fedha)

Hili sawa

9. Hali ya kuwa unadaiwa kiasi fulani cha fedha ili kutimiza hadi yako fulani watu huita balansi au salio. Usahihi ni bakaa.

More Ubantu than usahihi.

10. Jini mkubwa ambaye husadikika kuishi kwenye miti mikubwa kama mbuyu huitwa subiani na wala si. pepo (Kinyamkela huwa ndiye pepo ambaye hupungwa/kufukuzwa kwa ngoma inayokesha)

Tell that to the evangelicals if it makes a difference.
 
ha ha ha ha kubokoa.....
hata mi naona ni matusi.....ha ha ha.
 
Back
Top Bottom