Matumizi sahihi ya nafasi ya upendeleo

Matumizi sahihi ya nafasi ya upendeleo

Massawejr

Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
19
Reaction score
23
Leo nikiwa mishemishe nilipata kusikia mahojiano ya msanii mone centrozone akielezea kuhusu issue ya nafasi ya upendeleo, ambapo anafunguka na kusema mwaka 2017 alipata kuandika ngoma yake na kipindi hikohiko alipata shavu la kutumbuiza katika jukwaa la fiesta chini ya marehemu Ruge Mutahaba ambapo anasema alipewa nafasi ya ku-perform kama mtu wa mwisho baada ya wasanii wote ku-perform na kwaupande wake alichukulia kama ndio nafasi ya dhahabu hasa ukizingatia alikuwa ndio anajitafuta na aliweza kufanya kitu cha tofauti sana na wayu wengi walibaki kushangaa ni nani huyu amefanya hivi.

Nafasi ile aliyopata ilimbadilisha sana kimaisha na watu wengi katika mitandao ya kijamii walianza kumfatilia. Hili limenipa funzo moja kwamba pale tunapopata nafasi ya upendeleo au tunapopata nafasi ya kufanya au kuonyesha uwezo wetu basi tutumie vizuri nafasi izo pengine zisiwahi kurudi tena kwenye maisha yetu.

Maandiko matakatifu yanasema ibada njema inaanzia nyumbani na mimi ninasema wewe ndio mchawi wa mafanikio yako.
 
Back
Top Bottom