Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
MATUMIZI YA NENO MHESHIMIWA (HONORABLE)
Yahusu kuheshimisha nyadhifa na majukumu kwa majina ya nyadhifa na kazi zao.
Waliosoma vyuo vikuu na kuchukia kozi ya rhetorical language watakuwa wamejifunza pia kipengere hiki na tungetazamia watumie jina mheshimiwa kwa usahihi na mahali pake.
Pia katika masomo ya waandishi wa habari, kisa hiki kitakuwa kimefafanuliwa kwa uwazi ili wawe wanaandika kwa usahihi zaidi.
Uheshimishaji majina ya nyadhifa na kazi na jina mheshimiwa
Neno honorable na kwa kiswahili mheshimiwa lina utaratibu wa matumizi ili kuleta maana halisi ya mheshimiwa (honorable).
Heshima kubwa ya kiongozi au mtumishi ni cheo chake na sio jina mheshimiwa.
Ufafanuzi wa matumizi wa jina mheshimiwa ni pale linapotumiwa jina lake (given name) hutangulizwa na jina mheshimiwa (honorable) ili kutofautisha na wengine waliopo wenye given name zinazofanana na kwamba jina linalotamkwa au kuandika ni la mtu mwenye wadhifa.
Mfano unapotaja jina Samia Suluhu, kwa kuwa watu watajiuliza huyu Samia Suluhu ni yupi, inatakiwa utangulize Mheshimiwa Samia Suluhu kwa kuwa ana wadhifa mkubwa, hata hivyo hiyo haitatosha lazima umalizie na wadhifa wake 'Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,' yaani Mheshimiwa Samia Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ukianza moja kwa moja na jina la wadhifa, mheshimiwa huwa omitted sababu jina Rais ni cheo cha juu kabisa na hadhi yake, hakuna mwingine zaidi yake, hivyo utatamka au kuandika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio hadhi na heshima ya pekee aliyo nayo na hakuna mwingine na ndio heshima kuu ya wadhifa wake.
Speaker wa bunge anayekalia kiti au naibu speaker huwa moja tu, na hivyo heshima ya speaker au naibu wake ni kiti anachokalia. Kuanzia na mheshimiwa Speaker ni kushusha hadhi ya wadhifa wake wa kipekee bungeni ambao ni Speaker wa Bunge. Ila ukianza kutaja jina lake Tuli Akson hapo inabidi utangulize Mheshimiwa Tuli na umalizie na Speaker wa Bunge la Tanzania. Ukitaja speaker haitakiwi kuanza na mheshimiwa Speaker, bali Speaker pekee ndio hadhi na heshima yake.
Hali kadhalika mawaziri na wabunge, nyadhifa zao ni heshima kubwa kuliko neno mheshimiwa na tunapotumia mheshimiwa waziri, mheshimiwa mbunge sio sahihi kwa kuwa kwa kufanya hivyo twatumia majina mawili ya hadhi ya mtu yule yule badala ya jina moja la hadhi ya mtu.
Vyombo vya vya ulinzi na usalama wana matumizi sahihi ya nyadhifa zao
Huwezi kusikia Mhesimiwa RPC, mheshimiwa Brigadia, mheshimiwa Major, mheshimiwa kamanda wa jeshi etc, bali huitwa kwa majina ya hadhi na nyadhifa zao za kikazi na hakuna matumizi ya jina mheshimiwa, ukitumia jina mheshimiwa badala ya jina la wadhifa wake unakuwa umeshusha hadhi na heshima ya wadhifa wake.
Majina ya heshima katika familia
Kila Moja atakushangaa ukisema mheshimiwa baba, mheshimiwa mama, mheshimiwa mjomba, mheshimiwa babu, mheshimiwa bibi nakadhalika, sababu heshima zao sio jina mheshimiwa, bali heshima na nyadhifa zao ni uzazi, yaani mama, baba, mjomba, shangazi, babu, bibi nakadhalika ndiyo yanayobeba heshima zao stahiki na nyadhifa zao.
Rhetoric (elimu ya usemaji) huainisha vizuri hayo yote vyuoni, nashangaa kwa nini tuendekeze mambo yaliyo kinyume na maana halisi pamoja na dhana ya heshima stahiki na kupachika majina yesiyoheshimisha majukumu yao kikazi na nyadhifa zao.
By Candid Scope