Mtambo 1272019
Member
- Jul 29, 2022
- 16
- 15
WENU MTAMBO1272019Maana ya simu janja.
Ni aina ya rununu ambayo inafanya mambo mengi kuliko simu nyingine ya kawaida,zinzfanya kazi kama tarakililishi,lakini hiki ni chombo kinachobebeka na kidogo cha kutosha katika mkono wa mtumiaji(Andrew Nusca;20 AUGUST,2009).
Matumizi ya simu janja yamepokelewa vyema na kukua kwa kasi sana katika nchi yetu. Sio ajabu kukuta wakazi wa mjini na vijijini wakitumia simu janja katika mambo mbalimbali. Ikumbukwe ya kuiwa , Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo watu wake wanatumia simu janja kwa wingi katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara. Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza kuleta matumizi ya simu janja ndani ya Tanzania .
Matumizi ya simu janja kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari yamekuwa yakipigwa vita sana,kwa hofu ya kuchochea kwa mmong”onyoko kwa maadili kwa wanafgunzi. Lakini, ukweli ni kuwa, hakuna maendeleo yajayo bila ya changamoto,hivyo lazima tutathmini na tuchukue hatua za kukabiliana na changamoto zitokanazo na matumizi ya simu janja, kisha turuhusu matumizi ya simu janja mashuleni kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita hadi chuo kikuu.
TAKWIMU ZA UKUAJI WA MATUMIZI YA ITANETI NA SIMU JANJA NCHINI TANZANIA
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,2017), idadi ya watumiaji wa intaneti mpaka kufikia disemba 2017, ilifikia watu millioni 23 ambayo ni sawa na 45% ya watanzania wote. Lakini pia kwa mujibu wa Millard Ayo;7 Juni,2021), watumiaji wa intaneti Tanzania walifikia milioni 29.
Takwimu za matumizi ya simu janja nchini Tanzania ni haba na zisizojitosheleza,ingawa naamini kupitia majibu yatakayo letwa na Sensa ya watu na makazi ya 2022,tunaweza kupata picha kamili na takwimu zilizojitosheleza juu ya watumiaji wa simu janja nchiniu Tanzania . ingawaje kutokujua idadi kamili hakuondoi umuhimu wa matumizi ya simu janja na intaneti mashuleni(mahsusi kwa wanafunzi kidato cha tano na sita ). Kwani ukweli ni kuwa kuna watumiaji wengi tu wa simu janja wakiwemo wanafunzi.
UMUHIMU WA MATUMIZI YA SIMU JANJA KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI (KIDATO CHA TANO NA SITA).
Naelewa wazi, kuna suala lqa matumizi mabovu ya simu janja na intaneti lakini hii imechagizwa na ukosefu wa elimu na maandalizi bora ya mapokezi ya maendeleo haya ya Tehama..Hivyo wacha niangazie, umuhimu kwa kurusiwa kwa matumizi ya simu janja mashuleni, lakini mahsusi kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita ilivyojadiliwa na kuchambuliwa hapa chini:
Simu janja na Intaneti humrahishia mwanafunzi kutafuta matini ya kujifunzia na kufundishia. Kutokana na ukuaji mkubwa wa intaneti na tehema,kumewezesha kuwepo kwa “Apps” kama vile “shule direct”,”letStudy”,” Msomi Bora” na “Website na Blogs “ ambazo zinajihusisha na utoaji wa matini ya kujifunzia . hivyo, kumruhusu mwanafunzi wa kidato cha tano na sita kutumia simu juanja na intaneti mashuleni,kutamuwezesha kujiondoa kwa utegemezi wa matini yatokayo kwa mwalimu pekee na vitabu vya kiada,hivyo mwanafunzi ataweza kutanua uwezo wake wa maarifa na ujuzi.
Kutawezesha na kumuandaa mwanafunzi kujiunga na elimu ya chuo kikuu na kuendana na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Ni ukweli usiopingika sasa, kuwa wanafunzi wengi wa elimu ya juu hujifunza na kufundishwa kwa kutumia intanenti na simu janja. Ukisikia “Assignments” na “projects” mbalimbali za chuoni, hufanywa kwa msaada wa intaneti na simu janja. Hivyo kuruhusu hili jambo, kutawawezesha wanafunzi kuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha wa kutumia intaneti na simu janja kwa matumizi sahihi ya kielimu hata waendapo kujiunga na elimu ya juu. Mijadala mbalimbali ya kitaaluma hufanyika kupitia simu janja (maalum kupitia whatsapp na telegram). Hivyo, ni wazi kuwa wanafunzi wengi wa sasa (vyuoni) wanaqpata shida juu ya matumizi sahihi ya intaneti na simu janja kwa sababu hawakuandaliwa vyema katika elimu walizopitia hgapo nyuma.
Vilevile, Simujanja na intaneti itamuwezesha mwanafunzi kutunza taarifa na nyaraka zake za muhimu za kielimu. Mwanafunzi ataweza kuhifadhi vitabu,matokeo yake ,risti za malipo shuleni,na vyeti vyake wa kitaaluma kupitia intaneti na simu janja. Kwa mfano, kupitia barua pepe”(e-mails)”,”Google Drive “ na njia nyingi salama zipatikanazo kupitia intaneti na simu janja. Nyakati za kutembea na nakala ngumu,begi lenye nyaraka za kielimu n.k unatutupa mkono katika ulimwengu wa sasa.
Itasaidia kujifunzia na kufundishia mashuleni kipindi cha majanga . kupitia ugonjwa wa korona uliopata nguvu na kuenea mwaka 2021, tulishuhudia wazi umuhimu wa matumizi ya intaneti na simu janja katika kufundishia na kujifunzia, kwani shule zote zilifungwa na kusitisha huduma za utoaji wa elimu kwa muda,ili kupunguza maambukizi, hivyo majanga yafananayo na hayo hayataweza sitisha mchakato wa utoaji wa elimu endapo matumizi sahihi ya intaneti na simu janja yataruhusiwa mashuleni. Msimu wa Korona tulishuhudia na kuingia kwenye wasiwasi mkubwa juu ya mustakabali wa elimu na wanafunzi wetu, kwasababu hatuna mazoea na matumizi ya intanenti na simujanja kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari umepigwa marufuku. Hivyo kuna haja ya kuruhusu matumizi ya simu8 janja na intaneti mashuleni.
Na kwakuhitimisha kuruhusu matumizi9 ya intaneti na Simujanja mashuleni ni hatua ya kuelekea na kufikia maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya 2025. Ili kuhakikisha kuwa tunafikia maendeleo ya Tehama nchini Tanzania , hakuna budi kuruhusu matumizi ya Intaneti na Simu janja Mashuleni (mahsusi kwa kidato cha tano na sita). Hii pia, itakuwa njia sahihi ya kuiwezesha Tanzania kuingia katika ushindania wa kidunia katika masuala ya Teknolojia ya Habari
ANGALIZO
Kabla ya kurusiwa matumizi ya intaneti na Simujanja mashuleni, lazima elimu ya kutosha na kampeni za matumizi sahihi ya intaneti na simu janja yafanyike nchi nzima, ili kuhakikisha watu(raia) na wanafunzi husika wanakuwa na uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa matumizi sahihi na jinsi gani ya kufanya matumizi sahihi ya intaneti na Simu Janja. Lakini, walimu lazima wakubali kubadilika kuendana na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, kwani walimu wengi wamekuwa wahafidhina “conservative”: watu wasitaka kubadilika kimtazamo na kiutendaji. Hivyo kuna umuhimu wa walimu kubadili mitazamo yao juu ya teknolojia.
“TEKNOLOJIA IKITUMIKA SAHIHI INA MANUFAA MENGI, TUITUMIE IPASAVYO”
Upvote
1