Vipi Emmanuel
Splitter, kama jina linavyoeleza ni mfumo unaotumika kw transmission/gearbox, kuipa uwezo zaidi wa kukidhii mzigo kw "kuivunja" kila ratio mara mbili, high na low; kwa undani ni kuongezea ratio kw kila gear. Uwezo huu ni kupunguza tofauti kati ya ratio/gear za ile transmission.
Inafaa nielezee ifanyavyo kazi transmission! Transmission hua na ratio/gear tofauti ili kurahisisha mzigo wa gari (uzani, shehena iliobebwa, ubadili kasi na muiniko wa barabara) kw engine. Kwa mfano, gear namba moja huiwezesha engine kuzunguka mara nane kwa kila mzunguko mmoja wa shaft inayotoka kw transmission kwenda kw diff. Hii ina maana gear namba moja ina nguvu na sio kasi; gear namba mbili nayo utapata inaiwezesha engine kuzunguka mara sita kw kila mzunguko mmoja wa output shaft. Tofauti ya hizi gear ni mzunguko mmoja, kw mlima mkali tofauti hii yaweza ilemea engine kuendelea na mwendo kw kua ni kubwa sana. Kabla ya kuweka ratio au gear nyingine pale kati ili kua nusu ya mzunguko, mfumo wa epicyclic train utumika kw transmission kurahisisha mzigo. Hapo ndio high na low uingilia kw kua kila gear ina high ambayo ni sababu ya ule mfumo wa epicyclic train/splitter kuiongezea mzunguko bila kuitoa ile ya kwanza kwenda ya pili na kukaribisha au kupunguza tofauti ya ratio za transmission.