Matumizi sahihi ya split gear.

Chacho Haulage

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2017
Posts
267
Reaction score
308
Wakuu naomba ufafanuzi juu ya matumizi sahihi ya spliter kwenye magar makubwa hii ni baada ya ubishi mkubwa uliojitokeza.. Wengine walidai unaweza tumia spliter kwenye gia zote kuanzia 1-6 kwa 12speed na 1-8 kwa 16 speed haijalishi gari ina mzigo au haina na wengine wakadai ni vizur spliter itumike katika high range pekee Kama gari ina mzigo nkaona n vema ntafute ufafanuzi bora kabsa mahali apa.. Naomba kuwasilisha
 
Vipi Emmanuel
Splitter, kama jina linavyoeleza ni mfumo unaotumika kw transmission/gearbox, kuipa uwezo zaidi wa kukidhii mzigo kw "kuivunja" kila ratio mara mbili, high na low; kwa undani ni kuongezea ratio kw kila gear. Uwezo huu ni kupunguza tofauti kati ya ratio/gear za ile transmission.
Inafaa nielezee ifanyavyo kazi transmission! Transmission hua na ratio/gear tofauti ili kurahisisha mzigo wa gari (uzani, shehena iliobebwa, ubadili kasi na muiniko wa barabara) kw engine. Kwa mfano, gear namba moja huiwezesha engine kuzunguka mara nane kwa kila mzunguko mmoja wa shaft inayotoka kw transmission kwenda kw diff. Hii ina maana gear namba moja ina nguvu na sio kasi; gear namba mbili nayo utapata inaiwezesha engine kuzunguka mara sita kw kila mzunguko mmoja wa output shaft. Tofauti ya hizi gear ni mzunguko mmoja, kw mlima mkali tofauti hii yaweza ilemea engine kuendelea na mwendo kw kua ni kubwa sana. Kabla ya kuweka ratio au gear nyingine pale kati ili kua nusu ya mzunguko, mfumo wa epicyclic train utumika kw transmission kurahisisha mzigo. Hapo ndio high na low uingilia kw kua kila gear ina high ambayo ni sababu ya ule mfumo wa epicyclic train/splitter kuiongezea mzunguko bila kuitoa ile ya kwanza kwenda ya pili na kukaribisha au kupunguza tofauti ya ratio za transmission.
 
Asante sana kaka unajua iv vyuma tunaendesha tu kwa kutumia uzoefu wa waliotufundisha so tunapopata darasa kama iv tunaongeza maarifa
 
So hakutakua na effect yoyote kama ntaamua kutumia high and low split katka ratio /gear zote no matter gari ina mzigo kiasi gani?
 
So hakutakua na effect yoyote kama ntaamua kutumia high and low split katka ratio /gear zote no matter gari ina mzigo kiasi gani?
Itategemea kama engine itaweza kuipokea ratio/gear unayoiweka bila kulemewa na mzigo - hapa ni unapopanda kw ratio/gear, au engine haitanyongwa kupindukia na ratio/gear unayoweka - hapa ni unaposhukà gear.
 
Split gear hutumika baada ya high range tu no matter gari ina mzigo au hapana ispokua madereva wengi wa kibongo huendesha kwa mazoea mradi split inakubali wao hudhani hvyo ndivyo sahihi
 
Split gear hutumika baada ya high range tu no matter gari ina mzigo au hapana ispokua madereva wengi wa kibongo huendesha kwa mazoea mradi split inakubali wao hudhani hvyo ndivyo sahihi
N effects zp znaweza kutokea iktumia ktk Low range bother
 
TATIZO SISI WATANZANIA TUNAFANYA VITU VINGI KWA MAZOEA AU KWA KUIGA NA HATUPENDI KUVISOMA VITU NA KUVIELEWA MAGARI YOTE JINSI YALIVYOTENGENEZWA KUNA MAELEKEZO JINSI YA KUYATUMIA NA UKITAKA KUJUA MIFUMO YA UINGIZAJI GIA KATIKA MAROLI MAELEKEZO YAPO KWENYE KIKINGA JUA AU SUNVISOR UTAKUTA MICHORO INAYOELEKEZA NI VIZURI KUIFUTA KWANI NDIO ITAFANYA MFUMO MZIMA WA DRIVETRAIN KUWA SALAMA INA MAISHA MAREFU,TAMBUA KUNA MIFUMO MINGI YA TRANSMISSION KUNA SPICER 16,EATON FULLER HII NI KWA AMERICAN HAWA WANA MPAKA 18 SPEED,I-SHIFT,H-PARTEN HII KWA EUROPEAN KUANZIA 8-16 SPEED,MUHIMU KUZINGATIA RPM SAHIHI KUFIKIA KABLA YA KUONGEZA AU KUPUNGUZA GIA HII NI KWA GARI ZOTE ZENYE MFUMO WA MANUAL TRANSMISSION MPAKA GARI NDOGO,SIJABOBEA SANA ILA KWA WANAOJUA ZAIDI WANISAIDIE.
 
Asante sana mkuu umeniongezea kitu sikuwahi kujua kwenye sunvisor kuna maelekezo pia.. Shida ni kwamba unapewa gar ambayo wameshaitumia watu kibao hakuna cha kijitabu, sunvisor ilishavunjwa kapo kakipande tu ndo maana madere wengi wanajikuta wakiendesha kwa mazoea ukilinganisha na madereva wachache waliopata mafunzo kupitia vyuoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…