Matumizi sahihi ya taa za gari.

Namba moja sijakupata...ila kwa namba 2 kama kuna mistari miwili katikati ya barabara na wa kushoto ni wa dash dash maana yake wew dereva unae kwenda mbele unaruhusiwa kulipita gari la mbele yako kama ni salama kufanya hivyo...lakini yule ambae anaelekea ulipotoka au unaepishana nae haruhusiwi kulipita gari lililopo mbele yake kwa sababu mstari wake ni wa moja kwa moja hauna dash. Hii yote imetokana na utaratibu kuwa kama mstari wa katikati ya barabara ni wa moja kwa moja yaani hauna dash dash ina maanisha hakuna dereva wa upande wowote anaeruhusiwa kulipita gari lililopo mbele yake....lakini kama mstari ni wa dash dash basi dereva anaruhisiwa kulipita gari la mbele KAMA ni salama kufanya hivyo.
 
Achana na mambo ya kucopy na ku paste bana me naongea kutokana na halisi ya mambo maana hiyo pdf ni tofauti na sheria za bongo umeona mataa ya bongo yanavyofanya kazi umeona ni sawa na UK??so ongea vitu ambavyo unajuwa na sio kukurupuka....

Nicheke mie, Watanzania tuache uvivu, hiyo document hata hujasoma unakurupuka tu, unatakiwa utafuniwe kila kitu, haya, Road Markings kuanzia ukurasa 162 nk, warning signs kuanzia ukurasa 47 na chochote kuhusiana na matumizi ya barabara, ulitegemea nikutafunie hata uji, Grow up! Hiki ndicho kinarudisha maendeleo ya nchi hii, hamtaki kusoma mnataka mambo rahisi mkifanyiwa mnakurupuka. Nilikwambia Wacha uongo kwa sababu ulisema full beam inatumika UK kukiwa na fog etc huo ni uongo, kuna fog lights kwenye magari siku hizi sio uongo wa kusema full beam ndio inatumika. Achana na mambo ya chupi kaka/dada weka hoja.



Fog lights kama hizi .... ..
BTW sheria za barabarani za Tanzania tumerithi kutoka kwa Uingereza. Tuna ajali nyingi kwa sababu wengi wa madereva hawana vigezo vya kuendesha magari na hawafuati sheria za barabarani. Watu wanakunywa pombe then wanaendesha magari, what stupidity is that?
 
Ningependa Traffic wawe wanawakamata Madereva Vilaza ambao hawajaui matumizi ya Taa,Utamkuta mpo kwenye foleni gari zimesimama jamaa wa nyuma kawasha full hadi balaa,utakuta mtu anapita sehemu ambayo ina mwanga mzuri kabisa lakini kawasha taa full,Ni kero sana,Dawa ya watu kama hao akiwa nyuma mgeuzie kioo cha juu kwenye roof kimmulike yeye,na njia ya pili kama akiwasha full na wewe mpige full tu basi.
 
Kuna road ambazo katikati n mstari wa njano pembeni ndo white hapo ni vepeeee
hata wewe unauliza mistari wakati unayo, si ujiangalie mwenyewe, au hauna mfereji hapo katikati.
 
Ok, nashukuru kwa majibu yako. Hata hiyo namba moja nimejiongeza nimeelewa itakuwa na maana gani.
 
Sio matumizi ya taa peke yake mkuu. Hata alama za barabarani ni tatizo kubwa sana na tatizo linakuwa kubwa kwenye maungio ya barabara.
 
Na pia naomba niongezee katika suala la uwashaji wa indicator za magari....kuna namna flani hivi madereva wengi tumekuwa tukiitumia hususani katika uwashaji wa indicator.
INDICATOR YA KULIA: Kipindi gari la nyuma yako inataka kukuovertake na dereva wa hilo gari akikupa ishara kuwa anataka kukuovertake, na wewe uliye mbele yake unaona kabisa eneo hilo sio zuri kwa kuovertake hususan kama kuna gari linakuja huko mbele au kama kuna tatizo huko mbele, wewe kama dereva wa gari la mbele yake unabidi uwashe hiyo indicator kama tahadhari na kumuonya.
INDICATOR YA KUSHOTO: Dereva wa gari ambayo inapitwa na gari lingine huwasha hii taa ya indicator ili kumweleza dereva wa gari linalotaka kumuovertake kuwa huko mbele kupo salama kwa hiyo anamruhusu aovertake.
 
Asante sana mkuu kwa somo hili. Umenifundisha vitu ambavyo nilikua sijui
 
ni ishara ya kuwa hukati kulia wala kushoto bali unanyoosha tu
Ni kosa kuwasha hazard( indicator zote )kwenye makutano ya barabara kama hukati kulia au kushoto huna haja ya kuwasha indicator yoyete wewe nyoosha tu.
 
Ndo zimepigwa marufuku hizo taa zako, sasa sijui utawashtua na nini labda uweke chemli sasa
hahaa sikusikia basi nitalifunika govi la canvas kama naenda masafa natoa govi imbombo palepale[emoji53]
 
Watumiaji wa full lights usiku unawazungumziaje..ama matumizi sahihj ya full lights yakoje,baadhi ya magari akikuwashia full unaweza pata ajali kabisaa
 
Mkuu naomba kuuliza na zile taa za full zinawashwa na madereva wakati wa mchana mkiwa mnapishana hasa kwenye highway tunapokwenda mikoani? Wengine wanazitumia kuuliza hali ya barabara huko unakotoka (anakokwenda) kama kuna traffic police au la? Sasa swali langu ni je namjibuje? Nawasha full muda mrefu mpaka tupishane au nawasha na kuzima haraka haraka? Hapo atatakiwa kuelewa nimemwambia nini sasa incase imeamua kutumia aina mojawapo (full muda mrefu mpaka tupishane au nawasha na kuzima haraka haraka)?
 
Mi nisaidieni kama kuna fundi au mtumiaji mdadisi wa pikipiki aina ya Boxer BM150 kuna pipe moja nimesikia wakiita bliza pikipiki ikiwa mpya ile pipe inakiplastic cheupe kimeziba je? Ndio inavyopaswa kuwa? Na kama sivyo nin nikifanye??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…