SoC04 Matumizi sahihi ya Teknolojia katika taasisi za umma

SoC04 Matumizi sahihi ya Teknolojia katika taasisi za umma

Tanzania Tuitakayo competition threads

Backbuner

New Member
Joined
Jan 23, 2024
Posts
3
Reaction score
2
Tanzania ni moja ya nchi ambayo haiwezi kukwepa matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuendeleza uchumi wake. Taasisi za umma zinaongoza kwa kuwa na huduma isiyoridhisha kwa upande wa teknolojia ukilinganisha na huduma za taasisi za binafsi.

Ni kweli hatuna uwezo wa teknolojia iliyo bora na ya hali ya juu zaidi. Je, teknolojia duni tuliyo nayo tunaitumia ipasavyo?

Ni kweli hatuna vifaa bora vya kufanyia kazi lakini je, hivi vifaa tulivyo navyo vinatumika kwa usahihi? Mtu mmoja aliwahi kusema "huna haki kudai kikubwa kama kidogo kimekushinda kutumia".

Tumekuwa wazuri kwenye kusimama na kusifia vifaa vyetu na huduma zetu kwenye vyombo vya habari lakini tukija kwenye uhalisia ni asilimia ndogo sana ya ufanisi unakuwepo kwenye hiyo kazi.

Kila hospital inayotumia mfumo kwenye kutoa huduma, serikali ihakikishe kuna mnara. Hii ni kusaidia upatikanaji wa mtandao(internet) muda wote ili kuwapunguzia wagonjwa kukaa kwenye msululu kwa muda mrefu bila huduma kupata kwa kuwa mtandao unasumbua kwa wakati huo kwa kuwa ukosefu wa mtandao ni janga katika hospital zetu hapa nchini, kitendo hiki huwaweka watu wakisubili huduma muda mrefu na kuzuia baadhi ya shughuli zao za kiuchumi. Aidha tuwe na mfumo wa dharula ili kuepusha usumbufu kwa wananchi na watoa huduma kwa ujumla.

Mgawanyo mzuri wa utendaji kazi katika taasisi za serikali uenende na wakati, kulingana na uwepo wa teknolojia huduma zote zipatikane popote katika ofisi za taasisi isihitaji mtu kusafiri umbali kufuata huduma makao makuu.

Mfano.Tuna ofisi za Nactvet katika Kila Kanda lakini katika kutoa huduma wote makao makuu ndio wanaopokea maombi ya kimtandao iwe ya usaili wa wanafunzi au hata ya kuomba matokeo(transcript), vyeti vinachapwa makao makuu na kusambazwa kwa usafiri inaweza kuwa mabasi au ndege.

Katika ustawi mzuri wa taifa na huduma nzuri kwa wananchi makao makuu wawe na mfumo mmoja ambao utasaidia ofisi zote kuchapa hivo vyeti kwani makao makuu wametengeneze cheti mtandao(soft copy) ili kupunguza gharama za usafirishaji.

Taasisi za kiserikali wawe na watu au kitengo maalumu cha/wa kushugulika na maswala ya kimtandao na hasa kwenye sehemu ambazo zinahusiana na kutoa huduma mfano kupokea maombi au malipo ili kurahisisha upatikanaji huduma kwa jamii.

Ofisi nyingi za serikali zimetumia gharama kubwa kuunda tovuti mtandao na kuweka mawasiliano lakini cha ajabu, unapiga mpaka uchoke, ni ofisi chache sana ambazo ziko hai katika teknolojia tunayoisema.

Tutoke kwenye takwimu za mdomoni twende kwenye takwimu za uhalisia, tukianzisha matumizi ya teknolojia fulani tuhakikishe tunaitumia ipasavyo kabla ya kuanza kitu kingine.

Serikali imetumia gharama kubwa kujaribu kuwahamisha waalimu katika sekta ya elimu ili kwenda kidijitali kwa kugawa vishikwambi, lakini ufanisi wake sio mzuri. Ili kuijenga Tanzania tuitakayo tunahitajika kuwa na usimamizi sahihi wa Mali za umma kwa matumizi sahihi katika kufanya mabadiliko chanya kwa taifa letu kwa ujumla.

Teknolojia inapokuwa lazima uharifu uzidi kuongezeka kulingana na teknolojia iliyopo. Tanzania tuitakayo lazima iwe na mifumo salama kwa ajili ya matumizi salama ya teknolojia. Mfano usalama katika biashara za kimtandao juu ya taarifa za watumiaji wa mtandao. Kwa ukaribu serikali inatakiwa kuhakikisha biashara zao ziko salama na mtandaoni ni sehemu salama kuuza na kununua bidhaa na hapo tutaongeza mapato kwa taifa.

Ufuatiliaji wa karibu na Sheria kali zichukuliwe kwa wahalifu wa kimtandao, mfano kudhibiti matapeli wanaotuma meseji za kitapeli, kwa kuwafatilia na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

Tunatakiwa tuiandae jamii yetu katika sura halisi ya jinsi ulimwengu unavokwenda na hasa vijana kuwa na matumizi sahihi ya teknolojia na sio kwa muktadha mmoja wa kuburudisha lakini katika nyanja zingine zikiwemo kilimo, elimu na hata ujenzi wa taifa pia hii itasaidia kujenga Tanzania ya vijana na wakazi wenye uelewa mkubwa juu ya matumizi sahihi ya teknolojia.

Tutumie teknolojia pia katika kutunza, kufundishia na kurithisha tamaduni zetu kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingini, teknolojia isiwe sababu ya kupoteza utamaduni kwa kuiga mambo ya kwetu na kupokea ya wengine. Baba wa taifa Mwl. JK Nyerere aliwahi kusema" taifa lisilo na utamaduni ni taifa mfu" hivyo Tanzania tuitakayo inatakiwa kuwa na utamaduni na asili yake ambayo tumerithi kwa wazazi wetu na tuendelee kuuishi utamaduni wetu na kuwaruthisha vizazi vijavyo pia.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom