Big L
JF-Expert Member
- Nov 21, 2022
- 502
- 820
Habari zenu wanajamvi,
Leo nimekuja na suala hili la matumizi sahihi ya vipaza sauti nikiwa naomba mawazo yenu na hoja zenu kuhusiana na hili.
Makanisani, Mikutanoni, kwenye sherehe mbalimbali na sehemu nyingine nyingi tumekuwa tukitumia vipaza sauti tena kwa kupokezana yaani unakuta kipaza sauti kimoja mnatumia hata watu 30.
Wataalamu wa afya na microbiology pamoja na watu wengine je hili lina athari yoyote ya kiafya? Na kama zipo ni zipi na kipi kifanyike ili kuzuia athari hizo?
Leo mimi nilikuwa kwenye sherehe fulani sasa kuna mtu alipewa kipaza sauti aongee jambo fulani kwa bahati mbaya alikuwa anaongea kwa kutoa mate mengi sana juu ya kile kapaza sauti na baada ya yeye ilifuata zamu yangu kiukweli nilishindwa kuvumilia nikiaenda kwa DJ kuzuga kama naongea nae nikatoa kitambaa nikafuta sehemu ya juu ya kile kipaza sauti kisha nikarudi kuongea sasa.
Naombeni michango yenu tafadhali najua itakuwa msaada pia kwa watu wengine humu jukwaani.
Big L.