sisi ni ndugu
Senior Member
- Sep 4, 2018
- 121
- 136
Natumai wote tu wazima. Naomba kueleweshwa katika hili, hivi AC katika gari inakula mafuta sana? Au ni wastani tu?
Majibu yaliyotolewa na wadau
Majibu yaliyotolewa na wadau
---Mkuu kwa kifupi jibu halipo straight foward. AC ya gari unatumia nguvu kutoka kwenye engine,no maana hata unapowasha AC muungurumo huwa unabadilika. Kwa hiyo unatumia mafuta zaidi,hiyo ni sehemu ya kwanza.
Sehemu ya pili ni kwamba unapofungua vioo haswa kwenye high speed ili kuokoa mafuta, upepo unaingia ndani na kusababisha 'drag' yaani gari inakuwa kama inazuiwa kwenda kwa sababu ya upepo unaojaa ndani na hapo inasababisha gari kutumia mafuta mengi zaidi ya unapokuwa umewasha AC.
kumbuka kuwa gari inapokuwa designed na kuwekwa kwenye "wind tunnel" madirisha huwa yamefungwa. kama umeweza kunua gari,sidhani kama suala la mafuta linatakiwa kukuumiza kichwa.Chagua sumu yako hapo.
Nipo kwenye hii Field. Uliyosema yana ukweli kabisa.
Nashauri tu kwamba wewe unaetumia A/C hakikisha mfumo wake uwe katika hali nzuri.
Kuna kifaa kinaitwa Compressor huwa kina engage na kudisengage kutokana na demand ya ubaridi ndani ya gari sasa kama mfumo wa a/c haupo vizuri kufikisha ubaridi unaotakiwa inamaana compressor yako itaengage kwa muda mrefu sana au moja kwa moja na hivyo kuweka mzigo kwenye injini kwa muda mrefu.
Pia hakikisha unafunga vioo na hakikisha pia seals kwenye milango na sehemu zenye upenyo zipo madhubuti ili zisiingize hewa kutoka nje ambayo ni ya moto vitavyofanya uhitaji wa compressor kuengage kwa interval fupifupi.
Otherwise Mfumo wa A/C wa gari ukiwa madhubuti hautaongeza sana Fuel Consumption ya gari lako.